WABUNGE WATAKA WEMA NA DIAMOND WASHITAKIWE KWA PICHA CHAFU MITANDAONI

Sakata la kusambaa kwa picha hizo
zisizokuwa na maadili mitandaoni
zikiwemo za watu maarufu hapa nchini
leo limeibuka tena bungeni likiwa na
sura mpya huku baadhiya wabunge
wakitaka kujua serikali inachukua hatua
gani juu ya picha zilizosambaa juzi
zinazomuonesha mmoja wa wabunge
(jina kapuni) akiwa na binti mdogo
ambazo mwenyewe alikanusha na kudai
si za kwake.
Moto huo ulizidi kuwaka bungeni leo
katika kipindi cha maswali na majibu
ambapo Mbunge wa Mchinga (CCM), Mhe.
Said Mtanda amehioji serikali
wamechukua hatua
gani dhidi ya vitendo vya uchapaji wa
picha zisizozingatia maadili huku
akiwataja Wema na Diamond kupiga
picha wakiwa chumbani na kuweka
kwenye mitandao.
Katika majibu yake Naibu waziri Habari
Utamaduni na Michezo Mheshimu
Mkamia, alijibu kuwa serikali imebaini
juu ya matumizi hayo ya picha
Mheshimiwa Habib Mnyaa aliuliza swali
la nyongea kwa wizara ya mawasiliano ya
sayansi na teknolojia ambapo jibu hilo
lilijibiwa na waziri wa mawasiliano
Katika majibu yake waziri wa
mawasiliano, sayansi na teknolojia Prof.
Makame Mbarawa anasema “Mhe. Spika
kuhusu picha zisizokuwa na maadili
zinazowekwa katika mitandao na watu
maarufu na hata wasiokuwa maarufu
serikali imeanza kuandaa kanuni
zitakazokuwa zikifuatilia Online Content
ambapo itaanza kuchukua hatua baada ya
kufuatilia juu ya picha hizo na kuchukua
hatua madhubuti”.
Baada ya kauli hiyo Spika wa bunge Mhe.
Anne Makinda alikazia akitaka majibu
juu ya picha za juzi zilizosambaa
zikimuonyesha Mhe. Komba akiwa na
binti mdogo ambazo mwenyewe alisema
si zake na wabunge kuonekana wakitaka
majibu ambapo Mhe. Mbarawa anasema.
“Mhe. Spika kuhusu picha za juzi
zilizosambaa mitandaoni tunazifuatilia
kujua zimeanzia wapi na taarifa zake
zikoje kwani hata mimi bado sijaziona ila
tutachukua hatua tutakapobaini
zilipotoka.”

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget