WEMA SEPETU ADAKA MIMBA YA DIAMOND PLUTNUMZ

'Beautiful Onyinye'  na kipenzi cha
Diamond, Wema Sepetu  sasa ni
mjamzito. Baada ya misukosuko ya
muda mrefu  ikiwemo  kuporwa na
wasichana wenzake penzi  lake la
Diamond, sasa Wema amepata kile
alichokuwa akikililia kwa muda
mrefu....
Chanzo cha habari hii kutoka kwa
marafiki wa Diamond kimedai kuwa
Wema amenasa ujauzito na
kugundulika hivyo walipokuwa Afrika
Kusini kwenye tuzo za MTV-MAMA na
kumfanya Diamond achanganyikiwe
kwa furaha....
Kwa mujibu wa chanzo hicho,
inadaiwa kuwa Diamond kwa sasa
kawa kama mtu aliyepagawa kwa
furaha kutokana na taarifa hizo njema
na tayari ameshaanza maandalizi ya
kijacho chake....
Kugundulika  kwa ujauzito wa Wema ni
baada ya kuanza kujisikia vibaya
walipokuwa Afrika Kusini ikiwemo
kichefuchefu na kizunguzungu
alipokuwa hotelini alipofikia na
kulazimika kwenda hospitali kwa
uchunguzi zaidi....
Inasemekana kuwa Wema alisindikizwa
na Aunt Ezekiel kwenda hospitalini
waliyekuwa naye huko Afrika Kusini
kumpa sapoti Diamond na madaktari
ndiyo waliomjuza kuwa anakiumbe
tumboni cha wiki 7...

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget