Rouhani: Iran ina azma katika mazungumzo ya nyuklia

 Rais Rouhani
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Tehran ina azma thabiti katika mazungumzo ya nyuklia na kwa msingi huo ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kutumia fursa iliyojitokeza kufikia mapatano kuhusu kadhia hiyo.
Rais Rouhani ameyasema hayo leo hapa mjini Tehran wakati alipohutubia kikao cha kiuchumi. Ameongeza kuwa dunia inapaswa kufahamu kwamba fursa iliyotolewa na Iran katika mazungumzo ya nyuklia si ya milele. Rais Rouhani amekumbusha kuwa mapatano ya mwisho kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran ni kwa maslahi ya pande zote husika. Akiashiria vikwazo vinaavyoongozwa na Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, Rais Rouhani amesema Iran imechukua hatua muhimu kukabiliana na vikwazo hivyo. Amesisitiza kuwa kuondolewa vikwazo ni kwa maslahi ya wote.
Ikumbukwe kuwa Iran na nchi za kundi za 5+1 ambazo ni Marekani, Ufaransa, Uingereza, Russia, China na Ujerumani zilifikia mapatano ya awali ya nyuklia mwezi Novemba mwaka jana. Hivi sasa pande mbili zinaendeleza mazungumzo ya kufikia mapatano ya mwisho ya nyuklia na hivyo kuhitimisha mgogoro wa zaidi ya muongo moja sasa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran wenye malengo ya amani.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget