Bwana Compaore sasa ametaka uchaguzi mpya
wa urais ufanyike baada ya siku 90.
Hata hivyo hakubaini ikiwa afisa huyo wa kijeshi
alikuwa akizungumza kwa niaba ya jeshi lote.
Jeshi lilisema kuwa litafanya mkutano na
waandishi habari.
Maelfu ya waandamanji walikuwa wamerejea
mabarabarani kwa siku ya pili
Siku ya alhamisi waandamanaji waliokuwa
wamekasirishwa na jitihada za rais za kuongeza
muda wa uongozi wake wa miaka 27
walitetekeza bunge na kuvamia kituo cha
runinga ya taifa.
Bwana Compaore alitupilia mbali jitihada za
kubadilisha katiba ambayo ingemruhusu
kuwania tena muhula mwingine kama rais lakini
akasema kuwa angebaki madarakani kwa
mwaka moja zaidi .
Post a Comment