Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiwa Ethiopi, leo ametangaza kutoa dola Milioni 100 kutoka mfuko wa kushughulikia majanga, CERF kwa ajili ya operesheni za usaidizi wa kibinadamu zinazokabiliwa na ukata ikiwemo Afrika.
Maeneo ya Afrika ni pamoja na Mashariki na Kati mwa bara hilo ambapo Ban amesema fedha zitasaidia mamilioni ya wahitaji waliolazimika kung'oka makwao kutokana na mizozo ikiwemo warundi 126,000 waliolazimika kuondoka kwao na kuelekea Tanzania tangu mwezi Aprili mwaka jana.
Tanzania ni moja ya wanufaika ambapo mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Alvaro Rodriguez amezungumza na Idhaa hii na kutaja kiwango itakachopokea na matumizi.
Post a Comment