PONA MARADHI YANAYOKUSUMBUA KWA KULA TUNDA,

                                                                         PERA
FAIDA 17 ZA MAJANI YA MPERA. (DAWA NI BURE LAKINI TUNAJINUNULIA MARADHI)

Mapera ni matunda ya msimu yenye wingi wa vitamini A na C, madini ya potasiam, nyuzi nzuri ya fiber na 'lycophene' vyote hivi ni muhimu kwa afya.

Watu wengi hutumia tunda tu pasipokujua si tunda pekee lenye manufaa kwa afya. Majani ya mpera ni mazuri kwa ajili ya ngozi, nywele na afya kwa ujumla. Ifatayo ni njia kadhaa za kutumia majani ya mpera kwa ajili ya afya yako.

1.Chai ya majani ya mpera inasaidia mwili kuwa stadi, inasaidia madini ya carbohydrates isigeuzwe kuwa sukari ndani ya mwili hivo kupunguza hamu ya kula.

2.Chai ya majani ya mpera pia inashusha kiwango cha sukari mwilini na kuzuia mwili kuondoa 'insulin'. Kwa sababu ya hii wagonjwa wa sukari wanashauriwa kuitumia mara kwa mara.

3.Chai ya majani ya mpera pia hupunguza lehemu mbaya(bad cholestrol) bila kudhuru lehemu nzuri.

4.Chai hii ina nguvu za kudhibiti vijidudu vya magonjwa mwilini hasa kuzuia magonjwa ya kuharisha na kipindupindu.

5.Chai hii inatiza mchafuko wa tumbo na pia inasaidia kukabili madhara yaletwayo na chakula chenye sumu.

6.Chai hii hutibu kukooa na kupumua kwa tabu.

7.Upatapo uvimbe wa fizi na maumivu mdomoni kama jino kuuma, tafuna majani ya mpera.

8.Kwa matatizo ya homa ya dengue, chemsha glasi mbili na nusu na majani ya mpera (kadiria majani 9) mpaka maji yabakie nusu ya ujazo wa awali.

9.Chai ya majani ya mpera imefahamika kutibu kansa na 'prostrate' kwa wanaume.

10.Chai hii inasaidia kwa wanaume wenye tatizo la kuzalisha (Infertility).

11.Ponda majani ya mpera na kuweka sehemu ya kidonda au iliyokatika kuondoa maambukizi. Kwa maumivu nje ya sikio tumia chai ya majani ya mpera. Tia matone ya chai hii iliyopoa kwenye sehemu iliyoathirika.

13.Majani ya mpera hupondwa na kupakwa eneo lenye muwasho uletwao na allergy.

14.Unapoumwa na wadudu majani yalipondwa ni tiba sahihi.

15.Majani ya mpera yana saidia kupigana na mba na chunusi kutokana na wingi wake wa vitamini C.

16.Kuondoa madoa meusi kwenye ngozi ponda majani ya mpera changanya na maji kiasi na upake badala ya dawa za kawaida.

17.Fanya kama na.16 kwa tatizo la ngozi kuzeeka mapema.

18.Majani ya mpera yanaondoa tatizo la kukatika kwa nywele. Chemsha majani kisha wacha yapoe na ukande kwenye paji na eneo la ngozi taratibu kwa dakika 15. Wacha kwa dakika 30 kisha usha na maji masafi bila shampoo au sabuni. Fanya hivo mara 3 kila wiki.

Wengi waniuliza namna ya kuitengeza chai ya majani wa mpera. Kuna namna mbili. Aidha chemsha maji kama glasi nne mpaka ikokote sana, chukua majani kama 10 ya mpera, weka ndani ya ule maji moto alafu funika kwa dakika 10 - 15 koroga chuja, chai yako tayari. Aina ya pili ni chemsha maji hayo pamoja na majani yakiwa ndani. Iki-kokota ondoa kwa moto, wacha kwa dakika 10 -15 chuja, chai tayar. Waeza tumia majani ulio kauka pia. Kabla nisahau ukichanganya na asali badala ya sukari ndio bora zaidi.
www.izabreez.blogspot.com
 

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget