IZABREEZ

Latest Post

Kitendo cha kukumbatiana sio tu kinaleta upendo na kuileta jamii pamoja bali kina faida kubwa za kiafya na kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa, watu hushauriwa kukumbatiana angalau mara 8 kwa siku.
Nimekusogezea hapa faida 10 za kukumbatiana.
1- Husaidia kupumzisha ubongo.
Kumkumbatia mtu unayemjali au kumpenda kunasaidia ubongo kuzalisha homoni inayojulikana kama OXYTOCIN ambayo huusaidia ubongo kufikia kiwango kikubwa cha kupumzika, pia homoni ya OXYTOCIN humsaidia mwanamke mwenye ujauzito kujifungua kwa usalama zaidi kwani hufanya mfumo wa uzazi kupanuka.
2 – Husaidia mwili kupambana na magonjwa
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali watu wengi hasa wazee wanaokumbatiwa mara nyingi huwa na asilimia chache za kukumbwa na magonjwa kuliko wale ambao hawakumbatiwi, hivyo watu hushauriwa kukumbatia wazazi wao kwani hii itawasaidia miili yao kuzalisha kinga ya kupambana na magonjwa.
3 – Kukumbatiana husaidia kupunguza maumivu
Madaktari hushauri kuwakumbatia wagonjwa wetu kwani kitendo hicho kidogo kinasaidia ubongo kuachia homoni  inayojulikana kama endorphins ambayo husaidia kufunga njia zote katika ubongo ambazo hutuma taarifa ya kuwepo kwa maumivu kwenye mwili.
4 – Husaidia watu kuwa na mood nzuri
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali watu wenye hasira au mood mbaya kila siku huzalisha homoni chache sana za Dopamine na Serotonin ambazo zinasaidia kufanya ubongo kuwa na uchovu na kukosa furaha hivyo kumkumbatia mtu unayempenda inasaidia kuzalisha homoni hizi kwa wingi.
5 – Kukumbatiana huongeza ufahamu kwenye ubongo
Watu wanashauriwa kuwakumbatia watu wenye uzito wa kuelewa mambo kwa haraka hasa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa kama  Autism na Dementia kwani kitendo hiki husaidia ubongo kuzalisha homoni ya oxytin inayosaidia ubongo kuelewa jambo kwa haraka na kutatua maswali magumu.
6 – Hupunguza msongo wa mawazo
Kukumbatiana kunasaidia kupunguza uzalishaji wa homoni inayoitwa Cortiso ambayo husaidia ubongo ku-relax. Homoni hii ikizalishwa kwa wingi kwenye ubongo wa binadamu husababisha hutawaliwa na mawazo hasi yanayopelekea msongo wa mawazo.
7 – Humsaidia mtu kupunguza hofu
Tafiti iliyofanywa na Psychological Science Journal imeeleza umuhimu wa kumkumbatia mtu mwenye hofu kwani inasaidia ubongo kupuuza taarifa hasi zinazotumwa kwenye ubongo pia husaidia mtu kuzalisha homoni zitakazomfanya ajiamini.
8 – Huepusha mtu kupata magonjwa ya akili
Kukumbatiana kunasaidia kuzalisha kwa wingi homoni ya Dopamine ambapo uzalishwaji wa homoni hii husaidia ubongo kupambana na magonjwa ya akili kama Depression, Bipolar pamoja na Dementia pia homoni hii inasaidia mtu kujiamini na kuwa mkweli.
9 – Husaidia kuepusha magonjwa ya moyo
Utafiti uliofanywa North Carolina umesema kuwa watu ambao hawajaonana na wapenzi wao kwa muda mrefu mapigo ya moyo huongezeka kwa mapigo 90 kwa dakika ambapo hali hii sio nzuri kwani binadamu mwenye afya imara hupata mapigo 40 kwa dakika moja.
10 – Husaidia kupumzisha misuli ya mwili
Kukumbatiana kunasaidia kupumzisha misuli ya mwili ambapo watu wengi wanapokumbatiana hulegeza misuli yote iliyokaza na kusaidia mwili kupumzika. Hii ndiyo maana wazazi wengi hushauriwa kuwakumbatia watoto wao wanapoamka asubuhi na kabla hawajalala
sourse: millardayo.com

Kukuwa kwa teknolojia hasa ya simu kumesaidia kurahisisha maisha ya watu wengi ambao wanakiri hawawezi kuishi bila Smartphones, leo March 29 2017 izabreez.blogspot.com imekutana na stori inayohusu matumizi ya mitandao ya kijamii katika maisha ya kila siku husababisha msongo wa mawazo kwa mujibu wa watafiti.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na American Psychological Association’s ni kuwa zaidi ya 99% ya watu wazima humiliki simu za mikononi aina ya Smart phones na 74% wanatumia mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, Instagram na Snapchat.
Wakielezea uhusiano uliopo kati ya mitandao ya kijamii na msongo wa mawazo Wanasayansi wanasema:>>>

Watu wengi hupata msongo wa mawazo kutokana na matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii kwa kuangalia simu zao kila wakati, kutamani vitu ambavyo hawana kwa kuona kwa watu wanaowafollow katika mitandao na kupata hofu kubwa inayoweza kupelekea kupata msongo wa mawazo”
sourse:millardayo.com

Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuvamia ofisi za Clouds TV na kuwalazimisha watangaza wa kipindi cha Shilawadu kurusha kipindi kinachomuhusu Askofu Gwajima kikiwa hakijamaliziwa maandalizi kinyume na taaluma ya habari, Leo March 22, 2017 Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limefanya kikao cha maamuzi dhidi suala hilo.
TEF pamoja na Club ya Waaandishi wa Habari Dar es saalam (DCPC) na Umoja wa Club za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) zimepitisha maamuzi matatu ikiwemo.
  1. Kulaani vikali vitendo vya RC Paul Makonda
  2. Kutoandika na kutangaza habari zozote kuhusu Paul Makonda kwenye chombo chochote cha Habari.
  3. Kumtangaza RC Makonda kama adui wa Uhuru wa Vyombo vya Habari pamoja na yeyote atakayeshirikiana naye.

Taarifa zinasema Bw Kaweesi ameuawa baada ya gari lake kumiminiwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa anaondoka kwake nyumbani Kulambiro, Kisaasi kaskazini mashariki mwa mji mkuu Kampala.
Walinzi wake wawili walioandamana naye pia wameuawa.
Bw Kaweesi aliteuliwa kuwa msemaji wa polisi Agosti mwaka jana.
Taarifa zinasema alikuwa njiani kwenda kuwahutubia wanafunzi katika chuo kikuu cha Uganda Christian University alipokumbana na mauti yake. Wanafunzi walikuwa tayari wamekusanyika ukumbini katika chuo hicho.
Miili ya watatu hao imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mulago
source bbcswahili 
picha hii ni kwa Hisani ya Izabreez.blogspot.com

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget