Jaji mkuu Willy Mutunga amesema hatatishika
Jaji mkuu wa Kenya Willy
Mutunga,ametangaza kuwa anatishwa na baadhi ya wanasiasa na mkuu wa
utumishi wa umma vitisho ambavyo anavitasfiri kama njama ya
kumshinikizwa kutekeleza maslahi yao.
Madai haya yanajiri wakati Kenya ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika chini ya wiki mbili.Aidha Jaji Mutunga ameelezea kuwa alipokea vitisho hivi karibuni wakati kesi iliyowahusisha mgombea wa urais Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto ilipokuwa inasikilizwa. Barua hiyo pia ilikuwa inawataisha majaji na mabalozi
Wawili hao ni washukiwa wa uhalifu wa kivita katika mahakama ya ICC na mahakama kuu ya Kenya wiki jana ilipaswa kuamua ikiwa washukiwa hao wanaweza kugombea urais au la.
Uamuzi uliotolewa na mahakama hiyo hata hivyo ulisema kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kuamua kesi hiyo na kwamba mahakama ya juu zaidi Kenya ndiyo ina uwezo pekee kutoa uamuzi.
Jaji mkuu Willy Mutunga alisema kuwa ujumbe wa barua aliyopkea ulikuwa unamtisha kuwa angetendewa jambo baya na kundi haramu la Mungiki ikiwa atatoa uamuzi wasioupendelea katika kesi ya wawili hao.
Uhuru Kenyatta na William Ruto wanakabiliwa na kesi ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya ICC
Mutunga aliituhumu serikali kwa kumfanyia dhulma baada ya kuamrishwa na afisaa mmoja wa uhamiaji kusafiri kwenda Dar es Salaam kwani hakuwa na idhini ya mtumishi mkuu wa umaa Francis Kimemia.
Bwana Mutunga alisema hatishiki na kuwa hahitaji idhini kutoka kwa Kimemia kabla ya kusafiri kwenda nje ya nchi.
Pia ameelezea wasiwasi kuwa majaji wanatishwa kisiasa huku nchi ikiwa inaelekea katika uchaguzi mkuu.
Mutunga amesema hatatishika kwani amekuwa mmoja wa wapiganiajai wa demokrasia Kenya na kwamba yuko tayari kwa lolote wanalompangia.
Chini ya uongozi wa jaji mkuu huyu, idara ya mahakama imeweza kusifiwa kwa mageuzi makubwa kwani sasa inaonekana kuwa huru na kuwa ni vigumu kuwashawishi majaji kuegemea upande wowote.
Mawakili nao wamelaani vitisho dhidi ya majaji na idara nzima ya mahakama wakiitaka serikali kuchunguza madai hayo.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.