HUU NI UNYAMA WA POLISI MAKETE WAUA MWALIMU KWA RISASI KISA HAKUVAA HELMENT YA PIKIPIKI YATAZAME MATOBO HAYO YA RISASI


HUU NI UNYAMA WA POLISI MAKETE WAUA MWALIMU KWA RISASI KISA HAKUVAA HELMENT YA PIKIPIKI YATAZAME MATOBO HAYO YA RISASI HAPA

--> 


Mwili  wa  mwalimu aliyeuwawa  kwa  kupigwa  risasi na  polisi Makete  kisa kutovaa Helment (kofia ya  pikipiki),tunaomba  radhi kwa  picha  hizi 
  Hivi  ndivyo mwalimu  wa  sekondari ya Kitulo  Casto Sote Kawamba alivyouwawa na  polisi 
Tunaomba Ladhi kwa picha za kutisha na endelea kutembelea mtandao huu kwa habari zaidi

............................................................................................................................................................

Mwalimu mmoja wa shule ya sekondari kitulo wilayani makete aliyefahamika kwa jina la casto sote kawamba ameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi Makete

Akizungumza na  mtandao  huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com  mkuu wa polisi wilaya yaMakete SP Peter Kaiza kuhusu tukio hilo lililotokea eneo la benki ya NMB tawi la Makete jana majira ya saa moja na robo alisema  kuwa mwalimu huyo alikuwa anakwenda kupata huduma za kibenki kupitia mashine ya  kutolea  pesa ya ATM akiwa na pikipiki ndipo alipo amuliwa na askari mmoja aitwae Jose Msukuma  na  kukutwa na umauti  huo .

 Inadaiwa  kuwa kisa cha mauwaji yake ni madai kutovaa kofia hiyo na baada ya  kuitwa na askari hao alikaidi amri na kutaka kumgonga askari huyo aliye kuwa lindo.

Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Idd Nganya ambaye ndie mwajiri wa marehemu amesema kuwa mwili wa marehemu bado umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya makete wakati utaratibu wakusafirisha mwili huo kwenda kwao mbeya kwa ajili ya mazishi ukiendelea

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye jina lake limehifadhiwa amesema kuwa askari hao walikuwa wakiomba fedha kwa mwalimu huyo na baada ya kukataliwa ndipo walipo anza kumshushia kichapo na alipo wazidi walilazimka kutumi asilaha na kumpiga begani kwa risasi  

Walimu wenzake na marehemu ambao walifika hospitali kujua kuhusina na kifo cha mwalimu mwenzake wameeleza  kusikitishwa na tukio hilo  na kulifananisha na tukio la kikatili machoni pao 

Mganga mkuu mfawidhi ambaye ni msemaji wa hospitali ya wilaya ya makete Dr Michael Gulaka amesema kuwa wao walipokea mwili wa marehemu na sio majeruhi

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget