HUU NI UNYAMA WA KUTISHA IRINGA , KIBAKA ACHOMWA MOTO AKITUHUMIWA KUIBA PAMPU YA TSH 25,000 TUNAOMBA RADHI KWA PICHA ZINAZOONEKANA!!!!!!!
mwili wa kijana Paul Raphael Mtekele ukiwa umefunikwa baada ya kuteketezwa kwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kuiba pampu ya kupulizia dawa mazao ya shilingi 25,000 katika kitongoji cha Tosamaganga B wilaya ya Iringa vijijini usiku wa leo
Viatu vya marehemu vikiwa vimenusurika moto na mwili wake kuteketea kwa moto
Mwili wa kijana huyo ukiendelea kuteketea kwa moto
Hivi ndivyo majeraha aliyoyapata kijana Kabla ya kuchomwa moto alipata mateso ya kukatwa katwa mapanga mwilini na kutaja orodha ya wezi wenzake
Baba Mzazi wa kijana Paul mzee Raphael Mtekele ( wa tatu kushoto akiwa ameshika kiono )
Mzazi wa kijana huyo mzee Raphael Mtekele
Wananchi wa njia panda ya Tosamanganga wakilitazama gari la polisi ambalo lilikuwa limefika eneo la tukio leo
Baba mzazi wa kijana huyo wa pili kushoto na polisi kanzu wakitazama mwili huo
Sanduku la kubeba mwili huo likiwa limeandaliwa baada ya mzazi kuwazuia polisi kuupeleka mwili huo Hospitali ya Ipamba kwa uchunguzi zaidi
...........................................................................................................................................................
WANANCHI wanaosadfikika kuwa na hasira kali wakazi wa njiapanda ya Tosamanganga wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa wamemuua kwa kichapo mtuhumiwa wa wizi kijijini hapo Paul Raphael Mtekele na mwili wake kuuchoma moto baada ya kijana huyo kuvamia nyumba zaidi ya mbili kijijini hapo na kuiba mali mbali mbali ikiwemo pampu ya kunyunyuzia dawa mazao yenye thamani ya Tsh 25,000
Tukio hilo la kinyama limetokea majira ya saa 9 usiku wa kuamkia leo katika kitongoji cha Kipanga B katika kijiji cha Njiapanda ya Tosamanganga wilaya ya Iringa vijijini jimbo la Kalenga .
Wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com leo eneo la tukio wananchi wa eneo hilo akiwemo Juma Mwakawago ambae pia katibu wa huduma za jamii kijiji hicho cha Tosamaganga amesema kuwa katika kijiji hicho kumekuwepo na matukio mbali mbali ya uharifu na watu kuibiwa mali na wanaodaiwa kufanya hivyo ni pamoja na marehemu huyo na kundi lake.
Hata hivyo kijana huyo kabla ya kuuwawa alikiri kujihusisha na matukio mbali mbali ya wizi kijijini hapo pamoja na kuwachomea nyumba wakazi wa eneo hilo na maeneo mengine pale wanapokosa kupata mali walizozifuata kwa ajili ya kuiba .
Pia alidai lengo lao kwa siku ya jana ni kwenda kuiba eneo la Ilula katika moja kati ya maduka ya mji huo wa Ilula ila wenzake waliopanga nao walichelewa kumfuata na hivyo yeye kuamua kufanya shughuli hiyo kijijini hapo na kuomba kusamehewa .
Alisema kuwa mbali ya matukio mbali mbali ya uharifu kujitokeza katika kijiji hicho ila usiku wa jana nyumba mbili za wakazi wa kitongoji cha Kipanga B zilivamiwa na wezi hao na kuporwa mali na kupelekea wananchi kufanya msako uliopelekea kumkamata kijana huyo akiwa katika harakati za kuvunja mlango wa nyumba ya mkazi mmoja wa kijiji hicho na baada ya kubanwa ndipo alipokwenda kuonyesha pampu hiyo iliyoibwa usiku huo.
Hata hivyo alisema kuwa baada ya kipigo kikali kijana huyo ambae sasa ni marehemu alilazimika kutoa orodha ndefu ya vijana ambao wamekuwa wakishirikiana katika uharifu ,orodha ambayo imehifadhiwa na wakati wowote kijiji kitaendesha msako wa kukamata mmoja baada ya mwingine.
Mmoja kati ya wazazi katika eneo hilo Delophina Mtavilalo ambae pia ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa vijijini alisema kuwa vitendo vya wizi katika kijiji hicho vimezidi na kuwa mbali ya wizi bado wanawake wamekuwa wakibakwa na kupokonywa mali zao .
Hivyo alisema tukio la kijana huyo kuuwawa mbali ya kuwa linasikitisha ila bado linapaswa kuchukuliwa tahadhari kubwa kwa vijana wanaoendelea kufanya shughuli za wizi na kuwataka vijana kuachana na shughuli hizo na badala yake kujiunga katika vikundi vya kiuchumi .
Mwenyekiti huyo wa CCM wilaya aliwataka pia wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaua watuhumiwa wa uharifu na badala yake mara baada ya kuwakamata wahakikishe wanawafikisha mbele ya vyombo vya sheria kwa hatua zaidi badala ya kuwaua kinyama kama hivyo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Njia panda ya Tosamaganga Dominic Ndenga alisema kuwa kijana huyo alikuwemo katika orodha ya vijana wanaojihusisha na vitendo vya wizi katika kijiji hicho.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa tayari kijiji kimefikisha taarifa kwa mkuu wa polisi wilaya ya Iringa (OCD) kumjulisha juu ya vitendo vya wizi katika kijiji hicho pamoja na unywaji wa pombe kupita kiasi ambapo wananchi wamekuwa wakishinda katika pombe usiku kuja na kuwa kuanzia sasa dawa yao inachemka .
Pia alisema orodha ya majina ya wizi iliyotajwa na marehemu huyo itafanyiwa kazi mara moja ili kuhakikisha mtandao wa uharifu katika kijiji hicho unakomeshwa na kuahidi kufufua ulinzi wa kijadi ( sungusungu )
Baba wa kijana aliyeuwawa mzee Raphael Mtekele alisema kuwa kijana wake alikuwa akituhumiwa kuhusika na vitendo vya wizi mara kwa mara na kupelekea kuhama kijijini hapo na kuhamia eneo la Ipogolo katika Manispaa ya Iringa na kuwa ni juzi tu ndipo aliporejea kijijini hapo na usiku wa leo kuuwawa .
Hivyo kuwataka wazazi kuendelea kuwaonya watoto wao kuachana na matukio ya wizi na kuwa iwapo watawatetea yaliyomkuta mtoto wake huyo pia yatawakuta .
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.