Kwa ufupi
Msanii anayetafuta mafanikio kwa kasi, Wema Sepetu amesema kuwa haoni sababu ya watu kutishiana maisha hasa kwa kipindi hiki ambacho maisha yapo juu.
Wema alisema hayo kufuatia hivi karibuni kutishiwa maisha na watu asiowafahamu na kulazimika kuongeza ulinzi nyumbani kwake na kila anapokuwa anatoka.
Alisema maisha ni magumu na kila mmoja anatakiwa afanye kazi kwa bidii ili kufikia malengo, badala yake watu wanaanza kutishiana maisha.
"Nawashangaa watu wanaoendelea kuwafuatafuata wengine wanapata wapi ujasiri huo na hali ya maisha ilivyo ngumu na kuhitaji muda mwingi wa kufanya kazi ili kujikwamua,"alishangaa Wema.
Aidha, aliongeza kuwa hana adui wala mtu ambaye anamdai au kitu kama hicho hivyo watu wanaomtumia mesaji za vitisho anahisi wana chuki binafsi na si kingine.
Post a Comment