Mtangazaji
mahili wa show za TV/Radio aliyeisimamisha wima show mpya na kali
inayorushwa kupitia channel 5 ‘Mkasi’ namzungumzia Salama Jabir ametupia
‘neno’ kupitia kipindi hicho kuwa huenda siku moja akaolewa na AY!
Kama
uliiangalia show ya Mkasi jumatatu ama marudio yake leo (jumamosi)
ambapo crew nzima ya kipindi cha mkasi chini ya C.E.O na Producer wa
show Ambwene Yesaya ‘AY’ walikuwa wakieleza changamoto na mambo
mbalimbali waliyokutana nayo wakati wanaanza kufanya kipindi hicho,
mwishoni Salama ambae alikuwa akimuelezea AY kuwa ni msanii ambae
anajivunia kufanya nae kazi kutokana na jinsi alivyomchapakazi na mtu wa
kuaminika alimaliza kwa kusema “huenda ipo siku moja tutaona..!”.
Wote
tunajua Salama alivyo mtu wa utani sana, kitu kinachoongeza burudani
ya ziada katika show zake, alitamka hivyo na kumgeukia AY akimuuliza,
na AY mwenyewe akajikuta anacheka na kukubali.
Pengine ulikuwa ni utani tu, lakini hakuna aijuae kesho ukizingatia wote wako single! source Jambo tz
Post a Comment