TUKIO LA KINYAMA HUKO JIJINI ARUSHA,MTU MMOJA AMWAGIWA TINDIKALI ASUBUHI NA MAPEMA AKIWA KWENYE GARI YAKE, HEBU SOMA HAPA

 
MTU mmoja mkazi wa eneo la Sakina jijini Arusha aliyefahamika kwa jina la JAPHET MINJA amemwagiwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni tindikali usoni na mkononi na watu wasiojulikana katika eneo la Shamsi kata ya Elerai na kumsababishia majereha.
Akizungumza katika hospitali ya Selian alikolazwa kwa matibabu MINJA ambaye ni fundi ujenzi amesema ametokewa na tukio hilo jana majira ya saa tatu asubuhi katika eneo la shamsi Drive in wakati akitoka nyumbaji kwake akiwa ndani ya gari ambapo alisimamishwa na watu waliomtaka kuongozana nao kwa ajili ya kufanya biashara na ghafla wakiwa njiani walimgeuka.
Daktari wa zamu aliyempokea mgonjwa huyo GODBLESS MASAWE amesema walimpokea jana asubuhi akiwa na fahamu lakini baadae hali ilibadilika na kulazimika kumpeleka katika chumba cha wagonjwa mahututi na kuwa kwa sasa hali yake inaendelea vizuri.
Jeshi la polisi mkoani Arusha kupitia kwa kamanda msaidizi ASP JAPTET LUSINGI amesema bado hawana taarifa kuhusiana na tukio hilo.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget