Akizungumza na Mwanaspoti jana Ijumaa, Malinzi aliahidi kupambana na watu wote wanaoleta vurugu uwanjani.
"Nitawashughulikia watu wanaoleta vurugu uwanjani," alisema Malinzi ambaye alichaguliwa kuwa Rais wa TFF Jumapili iliyopita.
Kauli ya bosi huyo ambaye zamani aliwahi kuwa Katibu wa Yanga, ni kama kuwanyooshea kidole mashabiki wa Simba ambao juzi Alhamisi walivunja viti Uwanja wa Taifa baada ya timu yao kubanwa kwa sare ya bao 1-1 na Kagera Sugar iliyosawazisha kwa penalti dakika ya mwisho.
Hata hivyo, Malinzi alisema kwa sababu ya uchovu wa kampeni ataondoka kwenda India kwa mapumziko ya siku saba.
"Ninaondoka Jumapili kwenda India kwa mapumziko ya siku saba, unajua tena kampeni zimenifanya nichoke," alisema.
Malinzi, ameahidi kupambana na mashabiki ambao wamekuwa wakifanya vurugu uwanjani akitolea mfano vurugu za mashabiki mechi ya Simba na Kagera, chanzo mjengwa
Post a Comment