NA
MAELEZO ZANZIBAR 02/11/2013
Wastaafu
wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC wametakiwa kutoa ushirikiano wao
pale unapohitajika ili kulifanya Shirika hilo kuzidi kusonga mbele.
Wito
huo umetolewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa ZBC Yussuf Khamis katika
Hafla maalum ya kuwaanga Wafanyakazi Wastaafu wa Shirika hilo
iliyofanyika Bungi Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema licha ya Wastaafu hao kuwa nje ya kazi ushauri wao utazingatiwa ili kuliimarisha zaidi Shirika hilo.
“Nakuombeni musijitenge moja kwa moja na Shirika kama mna ushauri wowote basi karibuni Ofisini ili kuliendeleza Shirika letu ”
Aidha Yussuf amewataka Wafanyakazi wa ZBC kuzidisha mashirikiano miongoni mwao ili kurahisisha utendaji kazi wa kila siku.
Kwa
upande wao Wastaafu hao waliushukuru uongozi wa Shirika kwa kuweza
kuwaandalia Hafla maalum ya kuwaaga jambo ambalo walidai baadhi ya
taasisi hawafanyi hivyo.
Aidha
waliiomba Serikali kuzidi kuyaboresha maslahi ya Wafanyakazi ili
Wanapomaliza muda wao wa kulitumikia taifa waweze kumudu maisha yao
vyema.
Katika Hafla hiyo Jumla ya Wafanyakazi Wanne waliagwa na kukabidhiwa zawadi baada ya muda wao wa Utumishi kumalizika.
Post a Comment