Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha, AJTC. Wamezua gumzo baada ya kuchanganywa na malipo ya mtaala Mpya unaotumika vyuoni kwa sasa.
Akizungumzia mkanganyiko huo Raisi wa chuo hicho bwana GEORGE SILANGE, amesema kuwa anachanganywa na malipo ya ada haswa kwa wanafunzi wanaotumia mtaala mpya kwani wamekua wakirudiswa ada mara kwa mara, kutokana na mpangilio usio rasmi vyuoni
Aidha Raisi huyo ameuomba uongozi wa chuo kufuatilia kwa umakini malipo hayo kwani yatakua yanapotosha wanafunzi wengi na kujikuta wakishindwa kuelewana na wazazi wao kwani wazazi hawakuwa tayari kulipa ada kama ilivyopangwa na uongozi wa chuo hicho
Hata hivyo chombo hiki cha habari kimebaini kuwa kuna hali ya kutokuelewana baina ya uongozi na wanafunzi ambapo ni hali inayopelekea mambo kama hayo kutokea, chanzo..izack mwacha
Post a Comment