Na izack mwacha.
Hivi karibuni niliweza kuzunguka na Kamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC) Manispaa ya Iringa na wilaya ya Iringa. Ilikuwa ni ya kutembelea maghala ya mbolea hasa ikiwa na lengo la kuangalia ufanisi wa usambazaji wa pembejeo kwa kutumia vocha. Mfumo huu wa matumizi ya vocha ni mzuri endapo wasimamizi wake watakuwa makini katika utekelezaji.
Tulipofika ghala la kampuni ya YARA eneo la viwanda la Ipogolo tuliweza kushuhudia mkaguzi wa mkoa wa Iringa anayemwakilisha Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG) akibanwa na wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake Deo Filikunjombe (MB).
Afisa huyu alishindwa kujibu maswali yaliyoulizwa juu ya upotevu wa vocha akidai kuwa ameshindwa kufanya hivyo kwa sababu kesi ziko mahakamani.
Mathalani aliulizwa mawakala gani wamefikishwa mahakamani? Fedha imetoka benki baada ya kuthibitisha kuwa vocha zimepotea? Ni maswali ya msingi ambayo kujua kama afisa mwandamizi ni msingi wako na hayaingilii uendeshaji wa kesi.
Ni vema kama wasimamizi wakuu au wakaguzi kujiridhisha kwa taarifa sahihi ili siku ikitokea yasiweze kukukuta.
Ni dhahiri kuwa kwa majadiliano yale niliyosikiliza kwa muda mfupi kuna matatizo katika usambazaji wa vocha na usimamizi wake.
Ni jambo la aibu afisa mwandamizi wa serikali unaposhindwa kujieleza kwenye masuala ya msingi ambayo yako wazi kwa maslai ya Taifa. Hakimu Mwafongo, Iringa
Post a Comment