LIVERPOOL imewaadhiri Arsenal waliokuwa wanasifiwa wana ukuta
mgumu, kwa kuwafumua mabao 5-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya
England jioni hii Uwanja wa Anfiled.
Mabao ya Liverpool leo yamefungwa na Skrtel dakika ya kwanza na 10,
Sterling dakika ya 15 na 52 na Sturridge dakika ya 20.
Bao la kufutia machozi la Arsenal lilifungwa na Arteta dakika ya 69 kwa
penalti. Ushindi huo, unaifanya Arsenal ibaki na pointi zake 55 katika
nafasi ya pili baada ya kuchea mechi 25, wakati Liverpool imefikisha pointi
50 baada ya mechi 25 pia, ingawa inaendelea kubaki nafasi ya nne.
Huruma: Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere akiwa haamini macho yake juu
ya kilichowakuta leo
Post a Comment