Ni muda mfupi tu toka Uganda ipitishe sharia
ya kupinga ushoga, imeripotiwa mtu mmoja
aliyetuhumiwa kuwa shoga alichomwa moto
mpaka kufa nchini humo.
CNN imeripoti tukio hilo ambalo jina la mtu
huyo halikuweza kujulikana. Picha ilionesha
jinsi mtu huyo anavyochomwa moto huku
akiwa pembeni mwa reli huku watoto
wakishuhudia tukio hilo.
Sharia hiyo iliyopitishwa hivi karibuni,
inahusisha pamoja na kufungwa maisha kwa
mtu yoyote atakayejihusisha na shughuli
zozote za ushoga pamoja na kuambukiza
ukimwi, matendo ya ngono na watoto pamoja
na watu wenye ulemavu, udhalilishaji ikiwa ni
pamoja na ubakaji.
Sharia hiyo iliyozaliwa mwaka 2009, na
kupewa jina “Kill The Gays” ikimaanisha “Ua
Mashoga” ambayo ilisisitiza hukumu ya kifo
kwa matendo fulani ya ushoga, lakini
ilirudishwa kabatini kutokana na kelele nyingi
zilizopigwa na mataifa mbalimbali.
Post a Comment