Baada ya tukio la Westgate ambalo
lilichukua maisha ya watu wengi,
jiji la Nairobi limekumbwa na
tishio jingine la aina hiyo kwenye
eneo la biashara la Nakumatt
Junction Barabara ya Ngong
ambapo yamekutwa masanduku
manne ya kubebea risasi kwenye
eneo la kuegesha magari kwenye
vyumba vya chini (Basement).
Masanduku hayo yalipatikana
ndani ya toroli la kubebea mzigo
kutoka kwenye duka la jumla la
Nakumatt ambapo walioshuhudia
wamesema sanduku hizo zilikuwa
zimeandikwa ‘e
xplosion’ na walipoitwa wataalam
wa mabomu wakagundua kuwa
sanduku ni za kubebea milimita 9
risasi za bunduki aina ya ceska
ama Mp5 machine gun.
Masanduku hayo yaligundulika
wakati wafanyakazi wakirudisha
matoroli hayo ndani baada ya
wateja kuyatumia na kuyaacha eneo la par king
Post a Comment