WATANZANIA 15 WAPEWA ADHABU YA KUNYONGWA BAADA YA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI CHINA

Matukio ya kukamatwa kwa
Watanzania nchini China kwa
kesi za biashara ya dawa za
kulevya yana idadi kubwa
sana ndani ya hii miaka mitano
iliyopita.
Miezi miwili iliyopita Balozi wa
Tanzania China alithibitisha
kwenye kwamba Watanzania
wasiozidi mia mbili ndio
wamefungwa kwenye magereza
mbalimbali ya China kutokana
na kesi tofautitofauti ila dawa
za kulevya ndio zinaongoza’
Balozi huyu alisema kwa
wakati huo hakuwa na rekodi
yoyote ya Mtanzania
kuhukumiwa kunyongwa au
yeyote ambae tayari
ameshanyongwa na kwamba
kwa taarifa zaidi Wizara ya
mambo ya nje itafutwe.
Baada ya hayo yote, hatimae
katibu mkuu wa wizara ya
mambo ya nje John Haule
March 25 2014 ametaja jumla
ya Watanzania waliokamatwa
kwa kesi ya dawa za kulevya
kwa kusema‘tuna Watanzania
wengi tu ambao wapo kwenye
magereza kule China japo
tumeshindwa kwa
harakaharaka kupata idadi ya
waliojihusisha na shughuli ya
dawa za kulevya lakini kuna
rekodi fupi tulizonazo sasa
hivi’
Katika Magereza ya China
mpaka February 2014,
tumepewa taarifa na Mamlaka
za China kwamba wapo
Magerezani Watanzania 177
ambapo 15 kati yao
wamehukumiwa kunyongwa
kutokana na biashara hiyo ya
dawa akini niseme tu wenzetu
wa Serikali ya China
wanatuthamini sana kama sisi
tunavyowathamini’
‘Wenzetu wa China
wanathamini zaidi uhusiano
wetu na ndiyo maana hata
wale wachache Watanzania
waliohukumiwa kunyongwa
hawajanyongwa mpaka leo na
hatutegemei kama
watanyongwa, yani sanasana
watafungwa kifungo cha
maisha gerezani’.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget