UFUMBUZI BUNGE LA KATIBA BADO FUMBO

MPAKA sasa haijulikani lini Bunge Maalumu la
Katiba litafunguliwa rasmi, kutokana na
kuendelea kusogezwa mbele kwa shughuli
muhimu za Bunge hilo kabla ya kufunguliwa
kwake.
Awali ilitarajiwa kwamba Rais Jakaya Kikwete
angefungua Bunge hilo kwa kulihutubia
Februari 24, lakini ilisogezwa mbele mpaka
Februari 28 na sasa haijulikani lini
litafunguliwa.
Wajumbe hao walikutana katika ukumbi wa
Bunge Dodoma kwa mara ya kwanza Jumanne
ya Februari 18 na tangu wakati huo, ratiba
imekuwa ikivurugwa na shughuli muhimu
kuwekwa kiporo.
Baada ya kuvurugwa kwa ratiba hiyo, sasa
Bunge hilo limeendelea kusogeza kazi zake
mbele kutokana na kuchelewa kupitishwa kwa
Kanuni za Bunge ambazo zimeendelea kula
siku kadhaa.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget