Makombora ya Lissu moto,, TBC yamzimia matangazo ya moja kwa moja ni kuhusu madudu ya muungano soma hapa

MAKOMBORA ya maneno
yaliyokuwa yakitolewa na msemaji
wa taarifa ya wachache bungeni,
Tundu Lissu, juu ya muundo wa
muungano, hati na nukuu
mbalimbali za viongozi wa kitaifa
yalisababisha kuvunjika kwa kikao
cha Bunge Maalumu.
Kuvunjika kwa Bunge hilo
kulitokana na taarifa zilizotolewa
kwa Mwenyekiti wa Bunge, Samuel
Sitta, kuwa Shirika la Utangazaji la
Taifa (TBC) lenye vituo vya redio
na runinga limekatisha matangazo
ya moja kwa moja (live).
Mjumbe wa Bunge Maalumu,
Freeman Mbowe, ndiye
aliyeanzisha hoja hiyo baada ya
kusimama na kuomba mwongozo
wa Mwenyekiti wa Bunge juu ya
hatua hiyo ya TBC kukatisha
matangazo yake wakati Lissu
akitoa ufafanuzi wa taarifa ya
walio wachache.
Mbowe alisema mjadala wa Katiba
mpya ni muhimu kwa taifa lakini
kituo cha runinga cha TBC
ambacho ni cha taifa kimekatisha
matangazo ya moja kwa maoja,
jambo linalowanyima fursa
wananchi kujua kinachoendelea
bungeni.
“Mheshimiwa Mwenyekiti naomba
mwongozo wako ni hatua au
jambo gani tutalifanya baada ya
televisheni na radio ya taifa
kukatisha matangazo ya moja kwa
moja ambayo imekuwa ikiyafanya
tangu tuanze mkutano huu,”
alisema.
Akijibu mwongozo huo Sitta,
alisema kuwa taarifa hiyo inashtua
kwakuwa Bunge limeingia
mkataba na serikali na TBC
unaotaka matangazo ya vikao vya
Bunge ni lazima yaonekane na
kufika kwa wanachi.
Sitta, alisema walifanya hivyo kwa
kuwa mchakato wa uandikaji wa
Katiba mpya ni shirikishi hivyo
wananchi wana haki ya kushiriki
na kujua kila kinachofanyika ndani
ya Bunge.
“Naomba Katibu achunguze mara
moja kuhusu kukatishwa kwa
matangazo ya TBC tujue kuna
tatizo gani kwakuwa jambo hili
linawanyima wananchi haki za
kusikia na kuona kile kilichotokea
hapa bungeni,” alisema.
Mara baada ya taarifa hiyo, Sitta
aliwataka wajumbe watulie kwa
muda afuatilie jambo hilo na
atawapa taarifa baada ya muda
mfupi.
Baada ya dakika chache Sitta
aliwaambia wajumbe kuwa
amepata taarifa kwamba hali ya
hewa Dar es Salaam ni mbaya
kutokana na mvua kubwa
iliyokuwa ikinyesha hivyo kuathiri
matangazo ya moja kwa moja ya
vituo vya runinga na radio vya
TBC .
Sitta alisema kutokana na kukatika
huko kwa matangazo ya moja kwa
moja, Bunge Maalumu haliwezi
kuendelea na mijadala yake kwa
kuwa wananchi watakosa fursa ya
kuona na kusikia kile
kilinachojadiliwa.
“Kwa sababu yoyote ile hatuwezi
kuendelea, natoa maelekezo kwa
Katibu kuangalia muda ambao
matangazo yaliyokatika na
alipoishia Lissu, wakati jambo hilo
likitokea….., ninawahakikishia
tukianza kikao Jumatatu mtu wa
kwanza atakuwa Tundu Lissu,”
alisema.
Mara baada ya kutoa kauli hiyo
wajumbe kutoka vyama vya
upinzani walikuwa wakishangilia
huku wengine wakipiga vigeregere
na kuimba: “Sitta….Sitta….Sitta
wewe ni Mwenyekiti wa viwango
na leo ndiyo umetuonyesha
viwango vyako.”
Uamuzi huo, ulionekana kumkera
Hamisi Kingwangala, ambaye
alisimama na kutaka utaratibu
akitumia Kanuni ya 52, (8), kuhoji
kanuni ipi iliyotumiwa na Sitta
kuahirisha Bunge kabla ya muda
unaotakiwa ilhali pia halikuwa
limemaliza shughuli za siku
husika.
Kigwangala alisema Kanuni ya 32
inazungumzia mijadala au
ufafanuzi wa taarifa za kamati
lakini hakuna hata eneo moja
linataja kuwa shughuli za Bunge
zinaweza kuahirishwa kwa sababu
ya kituo fulani hakijaonyesha
matangazo ya moja kwa moja.
Kauli hiyo iliwafanya wanjumbe
wenzake wamzomee huku
wakimuita msaliti lakini
Kingwangala aliwajibu: “Haya
ndiyo matatizo ya Bunge Maalumu
kuwa na wanasiasa makanjanja.’
Sitta amkata maini
Akitolea ufafanuzi Mwenyekiti wa
Bunge, Samuel Sitta, alisema
jambo linalofanyika hivi sasa
katika Bunge Maalumu ni kubwa
sana ndiyo maana limewekewa
bajeti ya kuwashirikisha kwa
kupitia vyombo vya umma
vinavyolipwa fedha.
“Wananchi wanaofuatiliana kwa
hamu yanayotokea hapa ndiyo
maana tunasema Bunge Maalumu
ni shirikishi sasa kama wananchi
hawaoni huo ushirikishi unatoka
wapi?
“Mimi nataka kutenda haki na
ionekane imetendeka, hivi
matangazo yamekatika na watu
hawaoni utawezaje kuzuia hisia za
wengine kutotendewa haki?
Tukiendelea itatafsiriwa kuna
ubaguzi fulani….mimi sitaki niwe
mbaguzi, nimeapa kutenda haki,”
alisema.
Sitta alibainisha kuwa ametumia
kanuni ya 85 ambayo inampa
mamlaka mwenyekiti kuamua
jambo au kuvunja kanuni kutokana
na sababu mbalimbali.
“Mimi nataka kutenda haki,
msemaji yeyote ikitokea hali kama
ya leo nitasitisha kidogo na
tutaendelea tena hapo baadaye….
katika kulifanya hilo sitajali vyeo
au kundi fulani,” alisema.
Mara baada ya kauli hiyo ukumbi
wa Bunge ulilipuka kwa vifijo na
vigeregere kutoka kwa wajumbe
waliokuwa wakimshangilia Sitta,
kwa uamuzi waliouita wa busara.
Hoja za Lissu
Awali Lissu wakati akianza
kusoma maoni ya walio wachache,
yaliyokuwa yametawaliwa na
nukuu za viongozi mbalimbali
pamoja na vitabu alivyokuwa
navyo, alisema waliozoea vya
kunyonga vya kuchinja hawawezi,
waliozoea vya haramu vya halali
hawawezi.
Alisema walipeleka mapendekezo
kwamba maoni ya wachache
yasomwe na wachache lakini
waliozoea vya haramu
wakayakataa kwa hoja kuwa
wanataka wayasome wao kama
watakavyosoma yao.
Kauli hiyo ilimfanya Sitta,
kumkatisha na kumtaka aache
kuwatuhumu wenzake waliomo
ndani ya ukumbi wa Bunge ambao
wamekwenda pamoja.
“Sisi sote tumekuja pamoja
kuwaita wengine kuwa wamezoea
vya haramu unaamua wewe,
hututendei haki hata kidogo
kwasababu ya usioelewana nao
basi wamezoea vya haramu, sasa
mjadala hauwezi kwenda hivyo,
ondoa hayo maneno ya waliozoea
vya haramu,” alisema Sitta.
Baada ya maelekezo hayo Lissu
alikubali kuyaondoa na kuingiza
mengine ambapo alisema
waliozoea kuishi kwa uongo na
udanganyifu hawawezi kujifunza
kuishi katika kweli.
Lissu alisema Katika kitabu
kinachoitwa Panafricanism cha
Profesa Issa Shivji katika ukurasa
93 wa kitabu chake amesema
kwamba hati ya makubaliano ya
muungano haikuwahi
kuthibitishwa na Baraza la
Wawakilishi Zanzibar kwa miaka
yote 50 tangu muungano uzaliwe.
“Alibainisha kuwa nyongeza zote
za mambo ya muungano tangu
mwaka 64 hadi leo ni haramu na
ni batili lakini leo Shivji ndiye
mpiga debe mkubwa wa CCM na
muungano huu wa serikali mbili,
mfano wa pili uko katika kitabu
kinaitwa ‘Tanzania’s 8th
Constitutional Amendment and its
implications of constitutionalism
democracy and union question,’
kilichoandikwa na Dk. Mwakyembe
1995”
Alibainisha kuwa Dk. Mwakyembe,
aliandika kitabu hicho kama
sehemu ya shahada yake ya
uzamivu ya Chuo Kkikuu cha
Humbarg, Ujerumani na kwenye
kitabu chake alisema kuwa hoja
ya Dkt. Wolfgang Dourado kuhusu
muungano kiuhalisia hati ya
makubaliano ya muungano
ilitengeneza muundo wa serikali 3
lakini utekelezaji wake umekuwa
tofauti, ukurasa wa 184.
Lissu alibainisha kuwa kwenye
ukurasa 195 Dk. Mwakyembe,
alisema mfumo wa shirikisho la
serikali 3 kama ilivyopendekezwa
na tume ya Nyalali na kuungwa
mkono na vyama na makundi ya
upinzani unaonekana ndio njia
pekee katika hali ya sasa ya
Tanzania.
Alisema kitabu hicho kinasema
mfumo huo unaweza kutoa kile
ambacho kimekosekana kwa
utaratibu wa sasa yaani wa wazi
wa mamlaka kati ya nchi washirika
na kati ya muungano na washirika
wake.
Lissu alisema Dk. Mwakyembe ni
mjumbe wa kamati namba 4
aliyomo yeye na ni mmoja wa
wajumbe walio wengi katika
kamati hiyo wamekataa shirikisho
na wamekataa muundo wa serikali
3, ambao wamezoea kuishi kwa
uongo hawawezi kujifunza kusema
ukweli.
Aliongeza kuwa mfano wa tatu
unahusu walioandika kitabu
kitachoitwa ‘Mali kuhusu rasimu
ya katiba’ na kimeandaliwa na
wahadhiri wa sheria wa vyuo
vikuu 15 vya Tanzania ambapo
katika ukurasa wa pili wa kitabu
wamejadili rasimu hiyo inayobeba
muundo wa serikali tatu
wanayoitaka wananchi na
wanaunga mkono muungano
wenye muundo wa shirikisho
lenye serikali tatu.
Alibainisha kuwa mfano wa nne
unamuhusu baba wa taifa, Julius
Nyerere mwaka 1968,
akizungumza na gazeti la
Observer la London alizungumzia
habari za muungano kwa maneno
kuwa iwapo uma wa Zanzibar bila
ya ushawishi kutoka nje na kwa
sababu zao wenyewe wataona
kuwa muungano una hasara kwa
uhai wao hatowapiga mabomu,
kuwalazimisha, muungano
utakuwa hauna tena sababu ya
kuendelea iwapo washiriki wake
wataamua kuukana.
Lissu aliongeza kuwa mwaka 1984
Wazanzibari walipohoji muungano
Alhaji Abood Jumbe akafukuzwa
kazi amewekwa kizuizini katika
eneo la Mji Mwema jijini Dar es
Salaam anakoishi mpaka sasa
huku Wolfgang Dourado akawekwa
kizuizini na baadaye kupelekwa
Ghana. sourse tanzaniaa daima

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget