Ajali nyingine ya Ndege, hii ni ya saa kadhaa zilizopita Marekani.
Mpaka
sasa kuna habari nne kubwa za ndege ambazo zimetokea ndani ya kipindi
cha siku 9 zilizopita, kuna ajali ya ndege tatu ambazo ni ile ya
Malaysia, Mali na Taiwan ambapo kwenye kisa kilichofata ni cha ndege
moja kulazimika kurudi ilikorukia baada ya kijana raia wa Canada kusema
ana mpango wa kuilipua nchi yake kwa sababu anaichukia.
Sasa tukio jingine la saa kadhaa zilizopita ni kuhusu ndege ndogo ya
abiria ambayo imelazimika kutua kwa dharura ufukweni huko Venice Florida
Marekani baada ya kupata tatizo ikiwa angani na rubani kuona hakukuwa
na uwezekano wa kufika uwanja wa ndege alikofanya mawasiliano.
Kutua
huku kwa dharura kumesababisha kifo cha Mwanaume mmoja alikua akitembea
ufukweni huku mtoto wake wa kike akijeruhiwa vibaya kwenye hii ajali.
Rubani na abiria wake hawakuumia kwenye hii ajali ila mtoto wa kike
ambae anahisiwa kuwa na umri wa miaka 10 ndio ameumia sana na kukimbizwa
hospitali.source milladayo
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget
Post a Comment