Waislamu Kenya waadhimisha Idul-Fitr
Waislamu nchini Kenya leo Jumatatu wamejiunga na wenzao katika nchi
kadhaa duniani kuadhimisha sikukuu ya Idul-Fitr inayoashiria kumalizika
mwezi mtukufu wa Ramadhani. Sala ya Idd imesaliwa katika miji mbalimbali
ya nchi hiyo huku Waislamu wa jijini Nairobi wakikusanyika katika
uwanja wa Sir Ali kwa ajili ya ibada hiyo. Sheikh kuu wa msikiti wa
Jamia, Muhammad Swalihu, amesema japo Wakenya wanasherehekea iddi kwa
furaha lakini Wapalestina wanaadhimisha siku hii chini ya madhila na
manyanyaso makubwa kutoka kwa utawala ghasibu wa Israel. Kiongozi huyo
amesema watu wa Palestina ambao ndio walio katika haki watapata ushindi
dhidi ya wazayuni maghasibu. Punde baada ya Sala ya Idul-Fitr huko
Nairobi, Waislamu walifanya maandamano huku wakitoa nara za kulaani
jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget
Post a Comment