Serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina imesema kuwa mashambulizi ya Israel yanayoendelea huko Ukanda wa Ghaza ni kutangaza vita kwa wakazi wa eneo hilo. Nabil Abu Rudeineh msemaji wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina amesema kuwa, mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza ni kuwatangazia vita raia wa Palestina wakazi wa eneo hilo na kwamba ni utawala huo ndio utakaobeba jukumu la mashambulizi hayo.
Msemaji wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina ameyataja mashambulizi ya Israel dhidi ya Ghaza kuwa ni mauaji ya wazi ya umati dhidi ya watoto, wanawake na wazee. Abu Rudeineh amelaani mashambulio hayo ya Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Ghaza na kusema kuwa Wapalestina wana haki ya kujitetea kwa kutumia njia zote za kisheria.
Post a Comment