Rais Macky Sall wa Senegal amemteuwa Mohammed Dionne kuwa Waziri Mkuu Mpya wa nchi hiyo siku chache baada ya kumfuta kazi Waziri Mkuu wa zamani Bi Aminata Toure Ijumaa iliyopita. Rais wa Senegal alimfuta kazi Aminata Toure baada ya chama chake cha Alliance for the Republic kushindwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa katika mji mkuu Dakar na kwenye miji mingine kadhaa mikubwa ya nchi hiyo koloni la zamani la Ufaransa. Wakosoaji wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa, sera zinazotekelezwa na Rais Macky Sally wa Senegal zimeshindwa kuandaa ajira na kukuza uchumi wa nchi hiyo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.sourse, radio iran
Rais wa Senegal amteuwa Waziri Mkuu Mpya

Post a Comment