Watu sita nchini Iran waliokamatwa baada ya
kuonekana kwenye kanda ya video iliyokuwa
inaiga wimbo wa 'Happy' wake mwanamuziki
mashuhuri Pharrell William, wamehukumiwa
kifongo cha hadi mwaka mmoja jela kila mmoja
pamoja na adhabu ya kuchapwa mijeledi 91.
Wakili wa sita hao amesema kuwa hukumu hiyo
itaahirishwa kwa miezi sita ikmaanisha kuwa
watafungwa tu jela ikiwa watarejelea kosa hilo.
Kanda hiyo inaonyesha wanaume watatu na
wanawake watatu ambao hawajafunika vichwa
vyao wakicheza densi kwenye barabara na
katika
paa za nyumba mjiniTehran.
Kanda hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa
kijamii wa You Tube, imetazamwa na zaidi ya
watu milioni moja.
Wengi wa waliohusika kuitengeza kanda hiyo,
walifungwa kwa miezi sita , huku mmoja wao
akifungwa kwa mwaka mmoja, alinukuliwa
akisema wakili wao Farshid Rofugaran.
Mmoja wa watu waliokamatwa kwa kucheza
densi
Kanda hiyo kwa jina, "Happy we are from
Tehran"
ilifikishwa kwa maafisa wakuu nchini Iran
mwezi
Mei baada ya kutazamwa na watu 150,000
kwenye You Tube.
Waliohusika pia walikamatwa na kushitakiwa
kwa
kosa la kukiuka sheria za kiisilamu ambazo
zinawazuia wanaume kucheza densi na
wanawake na pia wanawake kutoka nje bila
hijab.
Baadaye washukiwa walionekana kwenye
televisheni wakijitetea kwamba wao ni waigizaji
walihadaiwa kushiriki katika kanda hiyo
Kukamatwa kwa vijana hao kulizia ghadhabu
kutoka anga za kimataifa huku watetezi wa haki
za binadamu wakianzisha kampeinii kwenye
mitandao ya kijamii kutaka waachiliwe.
Mwanamuziki Paharrel Williams mwenyewe,
ambaye wimbo wake huo, uliteuliwa kwa tuzo
la
Oscar, pia alieleza kukerwa na kukamatwa kwa
watu hao.
"inachukiza kwamba vijana waliokuwa tu
wakijaribu kujifurahisha wanakamatwa,''
aliandika
kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Post a Comment