Na Izack Boniface:
Kauli hii
imejidhihirisha hapa nchini Tanzania Baada ya kuona Waandishi wa Habari Wa
Serikali Pamoja na wasio wa serikali wakikimbizwa na mbwa wa polisi pamoja na
kupigwa bila sababu kikubwa zaidi ikiwa
ni kukatazwa kufanya majukumu yao ya kuiripotia jamii kinachoendelea katika
nchi hii change,
Ikiwa
waandishi wa habari wamesimama kama muimili wa Nne wa serikali Wanastahili
kueshimiwa japo wao wanatumia Camera wakati polisi wakitumia silaha kama
Bunduki,Mabomu, m’bwa Pamoja nza Zana
mbalimbali za kutulizia Ghasia huku wakisahau kwamba wao siyo kitu kama nchi
haitokuwa ikiheshim vyombo vya habari,
Nchini
Tanzania kumekuwepo na Muingiliano wa
madaraka kwani Hata Raisi akisimama kusema jambo Inawezekana Dhairi mtu
mwingine kusimama na kuitengua kauli ya raisi bila kuchukuliwa hatua kama
mkosaji, hii imedhihirika pia siku moja baada ya makamu wa raisi kuomba
ushirikiano baina ya serikali na vyombo vya habari pamoja na kueleza umuhimu wa
vyombo vya habari lakini siku Iliyofuata waandishi wa habari bila kujali umri
wao wakongwe na wasio wakongwe walichezea kichapo kutoka kwa jeshi la polisi
wakati wakijaribu kutekeleza majukum yao. “Tumewaambia
muondoke mmekataa sasa Tunafanya kweli” mmoja kati ya maofisa wa polisi
alisiyekuwa kwenye msongamano huo alisema kwa sauti ya juu..
Ili kutatua
tatizo ni lazima utafute chanzo cha tatizo hilo, asingekuwepo Kiongozi wa CHADEMA mh Freeman Mbowe
kusingekuwepo na mkusanyiko huo, kwaiyo kama jeshi la polisi lilikuwa na mpango
wa kufanya kweli wangefanya kwa Mbowe kabla hajafika katika makutano hayo,.
Kama
asingekuwepo kiongozi huyo hata waandishi wa habari Wasingepigwa hii inatia
uchungu sana hasa kwa wanahabari ambao wao hawajui kutumia silaha tofauti na
camera zao, “Natamani siku moja na sisi waaandishi tunyanyue mitutu tufundishane
adabu”Kwa hasira aliropoka mwaandishi mmoja Ambae nae alikuwa kwenye
mkasa huo
Katika
Historia ya nchi zote zilizopo Duniani haikuwai kutokea Polisi Wakawakosea
Nidham kwa kiasi hicho waandishi wa habari kwani wanatambua dhahir mchango wa
waandish katika kuhabarisha Umma, Lakini hili tatizo linashangaza kwa nchi ya
Tanzania ambayo kiuhalisia bado ni change.
Mfano wa
madhara makubwa ambayo yanajitokeza kutokana na kipigo kama hicho ni ule wa
Bomu lililorushwa kule Ruvuma na kuwajeruhi vibaya Askari wa Doria, sababu
zilizoelezwa ni kwamba Mahusiano baina ya madereva wa bodaboda pamoja na askari
mkoani humo siyo mazuri, na mahusiano hayo yalitiwa Doa baada ya kile
kinachodaiwa kuwa askari walimpiga risasi ya mguu Dereva mmoja wa bodaboda
jambo lililopelekea kuinuka kwa hisia nzito kwa madereva hao ni kwanini
hawadhaminiki mpaka kufikia kiwango cha kufyatuliana risasi,
Kutokana na
mahusiano hayo kutokuwa mazuri hakuna anayejua ukweli halisi mpaka hivi sasa ni
nani ambaeye amehusika katika urushaji wa Bomu hilo huko mkoani Ruvuma kwani
Mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini DCI ISAYA MMGULU alisema kwamba ni bomu lenye
uzito wa hali ya juu tofauti na watu wanavyolizungumzia,
Hayo ni madhara
ya matukio yanayoweza kujitokeza pia baina ya Polisi na Waandishi wa Habari,
Kisheria
kumpiga mtu bila ya kuwa na sababu ni Kosa na mtu anaefanya hivyo anatakiwa
achukuliwe hatua kwa nnchi yenye kivuli cha amani kama Tanzania lakini kauli
iliyotolewa na jeshi la polisi
ni kwamba Tunafanya kweli kwa sababu tumeagizwa na wakuu wangu, Hao wakuu ni
kina nani kwenye afya za watu ni vema nyie wakuu mjifunze kudhibiti tatizo
kabla halijatokea,
Kichwa cha
habari hii kinasanifu ukweli kwamba Nchi ya Tanzania ina viongozi wanaosimamia
sheria na taratibu lakini usishangae sana endapo, Wariri wa habari
UtamaduniVijana na Michezo kukaa kimya kwenye hili Ni kawaida sana Hata
waliomteka Absolum Kibanda ambaye ni mwenyekiti wa dawati la wahariri Tanzania hawajajulikana mpaka hii
leo na Hata kama kuna waliohisiwa, ukimya uliendelea kutawala ili jina kamili
la nchi yetu yenye Amani liendelee kuwa na mantiki zaidi,
Viongozi
husika katika hili ni vema mkaweka umakini wa hali ya juu kwa sababu hilo
tayari ni giza limepandwa ndani ya mioyo ya waandishi wa habari kwani mawazo ya
mwenziyo hayafanani na na unayoyawaza pengine leo nawaza hiki kesho nawaza
kingine,
Ee mungu
Ipiganie Tasnia ya Habari ambayo haina Baba wala mama Wajomba ndio pekee wanao
onekana kwa mbali..creadity by izabreez
Post a Comment