Mkuu wa Kituo cha Polisi Anusurika Kuuawa na Wananchi baada ya kufamaniwa akitaka Kumbaka Mwanafunzi wa kidato cha nne

Mkuu wa kituo cha polisi cha Nyamboge
kilichopo katika kata ya Katoma wilayani Geita
mkoani Geita amenusurika kuuawa na
wananchi wenye hasira kali baada ya kukutwa
akitaka kufanya mapenzi na mwanafunzi katika
chumba anachoishi mwanafunzi huyo(Geto).
Tukio hilo limetokea juzi Jumapili majira ya
saa tatu usiku ambapo wananchi wakiwa na
marungu na mikuki waliweka mtego wa
kumnasa mkuu huyo mwenye namba E 2837
Koplo Venance.
Akielezea tukio hilo binti huyo (jina
linahifadhiwa)(19) anayesoma kidato cha nne
alisema siku ya jumapili mkuu huyo wa kituo
alituma maaskari wawili wiki jana wakaenda
kumkamata.
"Hata sijui kosa langu,nilikamatwa nikalazimika
kwenda na nilipofika alianza kunilazimisha
natembea na mwalimu wangu,nilipokataa
nilianza kupigwa na kulazimishwa kuandika
maelezo",alisema mwanafunzi huyo.
Alisema baada ya kukataa kuandika maelezo
alipelekwa rokapu na muda mfupi baadaye
alifuatwa na askari mmoja kati ya wale
waliomfuata anapoishi, alianza kuandika
maelezo na kumlazimisha kusaini.
Alisema baada ya kugoma kuandika alipigwa
sana na kuamua kusaini kutokana na kutishiwa
kufungwa na baada ya kusaini aliitwa na OCS
huyo na kumwambia aende nyumbani lakini
arudi jioni ana shida naye ya muhimu sana
lakini hakurudi kutokana na kuchoka na kipigo
alichokipata kituoni hapo.
"Kutokana na mkuu huyo wa kituo kutuhumiwa
na mwanafunzi kuwa anamtaka kimapenzi
ilibidi awaambie wanafunzi wenzake na
wananchi na baada ya hapo wakatengeneza
mtego ili wamnase" ,walisema mashuhuda wa
tukio hilo.
"Siku ya jumapili mkuu huyo wa kituo
alikwenda nyumbani kwa mwanafunzi huyo na
kuomba wafanye mapenzi kwa kuwa wenzake
anaoishi nao hawakuwepo lakini aligoma
kufanya hiyo ", walisema mashuhuda wa tukio
hilo na kuongeza:
"Kutokana na mtego wa wananzengo,muda
mfupi wananchi waliokuwa wamemuona OCS
anakwenda kwa binti huyo walifika hapo na
kufunga mlango kwa nje na kuanza kupiga
mwano".
Walisema kufuatia hali hiyo OCS huyo alivunja
mlango na kutoka nje huku wanachi
wakimkamta na kuanza kumpiga lakini
aliokolewa na askari na kufikishwa katika kituo
kikuu cha polisi cha wilaya ya Geita.
Hata hivyo baadhi ya wanakijiji waliokuwepo
kwenye tukio hilo walisema OCS huyo
amekuwa na tabia mbaya sana kwa wanafunzi
wanaosoma katika shule hiyo kwa kuwatongoza
na wakikataa anawasingizia kesi au ndugu zao
hivyo kuomba serikali kumchukulia hatua kali
OCS huyo kwa kitendo hicho kiovu.
Diwani wa kata hiyo Josephat Komanya
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kulaani
vikali kitendo hicho na kuwaomba wanafunzi
wa kata hiyo kuendelea kuwataja viongozi
ambao wanawataka kimapenzi kwa nguvu.
Share 0

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget