Ni kwenye Kanisa la Paradise Internation
Ministries lililoko Karakata Ukonga jijini Dar,
mwanamke mmoja (pichani) anayedaiwa
mchawi alidondoka usiku wa saa saba na
kujikuta hawezi kutembea.
Tukio hilo lilijiri Septemba 13, mwaka huu
wakati waumini wa kanisa hilo wakiwa
wamezama kwenye maombi ya kufunga.
Ilidaiwa kuwa, waumini wa kanisa hilo wakiwa
katika maombi hayo, Nabii Gideon Parapanda
aliwahakikishia kuwa usiku huo kutatokea
mambo ya ajabu kufuatia maombi hayo.
Inadaiwa ilipofika saa saba usiku mwanamke
huyo akiwa na wenzake watatu, walidondokea
kanisani hapo na kusababisha taharuki kwa
waumini waliokuwa wakifanya maombi ndani.
Mwanamke huyo alikuwa na kitambaa
chekundu kikidaiwa ni hirizi, fimbo nyeusi
iliyozungushiwa shanga na alikuwa amejipaka
masizi mwilini.
Akizungumza na Uwazi, Nabii Parapanda
alisema watu hao walidondoka watatu, wawili
walifanikiwa kukimbia akabaki huyo mmoja
aliyejitambulishwa kwa jina moja la Aisha,
mkazi wa Mwananyamala A jijini Dar.
Baada ya tukio hilo vyombo vya ulinzi, askari
wa JWTZ na polisi walifika kwa lengo la
kuhakikisha usalama wa eneo hilo lakini nabii
huyo aliomba mtu huyo asichukuliwe hadi
atapofanyiwa maombi maalum.
Ombi la kiongozi huyo lilikubaliwa ambapo
Aisha alipandishwa madhabahuni na kukiri
kuwa alikuwa na wenzake watano lakini katika
kuanguka walikuwa watatu, wawili walifanikiwa
kukimbia bila kusema walikuwa wakitoka wapi
kwenda wapi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP
Mary Nzuki alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo
alisema:
“Ni kweli tukio hilo limetokea na watu
wameshuhudia, mwanamke huyo bado yuko
kanisani hapo kwa maombi.”
Post a Comment