Mwigizaji wa filamu nchini, Aunty Ezekiel
amekanusha uvumi ulioenea kuwa alikwenda
nchini Marekani akifuatana na Waziri wa
Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu .
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Aunty
alisema hadi sasa haelewi nia ya
wanaovumisha habari hiyo isiyokuwa na
chembe ya ukweli wowote.
“Mashabiki wangu wajue nilikwenda
Marekani kwa mwaliko wa Blogu ya
Vijimambo, ambao walitaka nikashiriki katika
sherehe yao ya kutimiza miaka minne,
wakati wote nilikuwa na mwenyeji wangu,
Lukasi Mkami,” alisema.
Mwigizaji huyo alisema akiwa Marekani
alipigiwa simu na waandishi wengi
wakimuuliza kuhusu ziara yake na aliwaeleza
ukweli ulivyo, lakini anashangaa kibao
kimemgeukia.
“Sijakaa Marekani siku 14 kama
inavyoelezwa, nimekaa kule siku 10 tu,
nimeenda tarehe 13 (Septemba) na kurudi
24.
Nilikutana na Nyalandu tarehe 13, Waziri
alikuwa mgeni rasmi, tangu usiku huo wa
hafla sikumwona tena na sijui kama
aliendelea kuwapo Marekani au aliondoka.”
Alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo, Waziri
Nyalandu alijibu kwa kifupi bila kufafanua
alichomaanisha akisema, “Waongo wote,
sehemu yao ni katika ziwa liwakalo moto.”
Aunty ni mmoja kati ya wasanii wa kike
nchini wanaofanya vizuri katika tasnia ya
filamu, ambayo imekuwa ikizidi
kuitambulisha Tanzania nje ya mipaka yake
kwa filamu zao tangu walipofanya mapinduzi
miaka ya 2000.
Post a Comment