Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amefika
mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu
ICC huko Hague, ambako anakabiliwa na
mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu.
Yeye ni kiongozi wa kwanza wa taifa kuwasili
mbele ya mahakama hiyo.
Kenyatta amefika mbele ya mahakama hiyo
baada ya waendesha mashtaka kuishutumu
serikali ya Kenya kukata kuwasilisha ushahidi
muhimu.
Kenyatta amekanusha madai ya kupanga na
kufadhili ghasia za kikabila nchini Kenya baada
ya uchaguzi uliokumbwa na utata mwaka
2007/2008.
Kikao cha leo kitatathmini ombi la upande wa
mashitaka la kutaka kuahirishwa kwa kesi hiyo
hadi pale serikali ya Kenya itakapoikabidhi
mahakama hiyo ushahidi unaohitajika kuhusiana
na mali ya Rais Kenyatta.
Upande wa utetezi nao unataka kesi hiyo
ifutiliwe mbali ukisema kuwa upande wa
mashitaka hauna ushahidi wa kutosha kwa kesi
hiyo kuendelea.
Kiongozi wa mashitaka Fatou Bensouda,
amewasili mahakamani akisema kesi hiyo iko
katika awamu muhimu sana.
Kenyatta ameamua kukaa kimya akimtaka wakili
wake kuongea kwa niaba yake.
Post a Comment