Usiku wa kuamkia leo ulikuwa ni usiku wa
bara la Afrika huku timu kadhaa zikijitupa
uwanjani kutafuta tiketi ya kufuzu kwa fainali
za mataifa ya Afrika yatakayofanyika mwakani
huko nchini Moroko.
Tunisia walikuwa wenyeji kucheza dhidi ya
Senegal, hadi kipyenga cha mwisho Tunisia
ikaibanjua Senegal bao 1-0.
Nao mabingwa wa kihistoria Misri walimenyana
na Botswana, hadi mwisho wa mchezo huo
wenyeji Misri wakaibuka kidedea kwa
kuwaangamiza wageni wao bao 2-0.
Mashabiki wa Ivory Coast walilazimika kulala
mapema baada ya timu yao kustushwa na D.R
Congo kwa kupokea kichapo cha nyumbani cha
mabao 4-3.
Katika mechi zingine Cameroon iliiadhibu Sierra
Leone kwa jumla ya goli 2-0, Togo wakafanikiwa
kuiburuza Uganda kwa bao 1 bila majibu,
Zambia nao wakaifurusha Niger kwa jumla ya
magoli 3-0 huku mabingwa watetezi Nigeria
wakarejesha matumaini ya kufuzu baada ya
kuibanjua Sudani kwa jumla ya mabao 3-1.
Nayo Ghana ikaizabua
Guinea kwa ushindi wa goli 3-1, huku Angola
wakiiangamiza Lesotho kwa kipigo cha mabao 4
kwa mshanago.
Katika viwanja vingine Cape Verde wakaibomoa
Mozambique bao 1-0, Mali ikachezea kichapo
cha mabao 2-3 kutoka kwa Ethiopia. Nayo
Algeria ikaikalisha Malawi mabao 3 bila majibu,
huku Gabon ikitoshana nguvu na Burkina Faso
kwa sare ya 1-1 na Bafana bafana ikajiweka
katika hatari ya kufuzu kwa suluhu ya bila
kufungana dhidi ya Congo.
Post a Comment