SiKU chache baada pedeshee Mkongo,
Mwami Rajabu kutangaza kuwa anamtaka
staa wa sinema Bongo, Elizabeth Michael
‘Lulu’ kwa gharama yoyote, mwigizaji huyo
ametoa jibu linaloonesha dhahiri kwamba
alikuwa radhi kumkubalia.
Staa wa sinema Bongo, Elizabeth Michael
‘Lulu’
Akizungumza na waandishi wetu mara baada
ya habari ya Mkongo huyo kuandikwa
gazetini hivi karibuni, Lulu alisema
kilichomshangaza kutoka kwa mwanaume
huyo ni kwamba hakutakiwa kuanika hisia
zake katika vyombo vya habari kama kweli
ana nia ya dhati, angemtafuta mwenyewe au
kwenda kujitambulisha nyumbani kwao.
“Namshangaa sana huyo Mkongo kwa kweli
kama angekuwa na mapenzi ya kweli
asingeyaeleza kwenye magazeti, angenitafuta
au angekuja nyumbani kwetu hapo
ningemuona kweli ananipenda,” alisema
Lulu.
Pedeshee Mkongo, Mwami Rajabu.
Staa huyo aliendea kumwaga chache kuwa,
kama mwanamke, anahitaji kupewa heshima
yake na kudai kuwa wanaume wengi wa sasa
wamejisahau kupindisha mila za Kiafrika
kufuata taratibu na badala yake
wanatanguliza fedha mbele.
“Nadhani watu wamesahau mila za Kiafrika
kabisa, huwezi kuwa na mapenzi ya dhati
kwa mwanamke halafu utumie rafiki au
vyombo vya habari umpate, hiyo inakuwa
siyo heshima kabisa,” alisema Lulu.
Post a Comment