Katika soka la Tanzania wachezaji ndiyo
huwajibishwa pindi timu inapofanya vibaya
uwanjani na si makocha kama ilivyo kwa nchi
za wenzetu. Popote pale duniani timu
inapofanya vibaya, Walimu na benchi zao za
ufundi ndio hufukuzwa kazi. Jambo hilo halipo!
Mchezaji hawezi kutuhumiwa kwa kusikia
maneno au kutokana na mahusiano ya ‘mtu na
mtu’. Hii ni tabia mbaya, ni ‘ uswahili ambao
ndani yake unabeba chuki za wazi’..
Matokeo mabaya ya timu katika michezo
mitano ya mwanzo msimu huu katika ligi kuu
yamehusika kuwaweka wachezaji hao
(Kiemba,Chanongo na Kisiga ) katika ‘ lawama’,
lakini ukweli zipo sababu za msingi ambazo si
za kimpira zilitotumika kuwahukumu .
Mara nyingi tumekuwa tukisisitiza klabu kuwa
na uwezo wa ‘ kuwasajili na kuwamiliki’
wachezaji kwa kutumia vyanzo vyao vya
mapato. Poppe ametumia nafasi yake mara
kadhaa kuonyesha chuki kwa baadhi ya
wachezaji , Kuna wakati alihoji hadharani kwa
nini Kiemba anapangwa katika kikosi cha
Samba! Kwa kiongozi hiyo si kauli ya kuongea
katika vyombo vya habari. Tazama siku chache
baada ya kiongozi huyo kutoa maneno hayo,
Kiemba amesimamishwa, si yeye tu,
Chanongo amekuwa ‘ akisingiziwa tu’ kuwa ‘
yeye ni Yanga’, huo ni uswahili. Kuna ushahidi
gani wa kuthibitisha hilo?. Sababu kubwa
iliyofanya Kiemba, Chanongo na Kisiga
kusimamishwa ‘ ni kutumika’, kwa maana ya
kuihujumu timu yao ifungwe. Katika hali ya
kawaida hadi kufikia hatua ya kuwasimamisha
ilipaswa uwepo ushahidi, na si kufanya uamuzi
mkubwa kwa sababu za ‘ maneno ya kusikia
mitaani’. Kelele za mashabiki kusema wachezaji
hao wanacheza chini ya kiwango si sababu ya
maana. Simba ina wachezaji wangapi?
Katika orodha ya wachezaji zaidi ya 25 kwa nini
kocha aamue kumtumia Chanongo pekee?.
Labda kama wachezaji wote katika timu hawana
uwezo ndiyo maana kocha anaamua kumtumia
Chanongo. Hili ni tatizo la viongozi wengi katika
soka la Tanzania ambao njia zao za kuingia
madarakani huwa si sahihi. Kuchaguliwa bila
sera hupelekea kuingia madarakani watu
wenye hela, ambao wanapofika katika nafasi
hizo huwashinda sababu ya kukosa ‘ sifa ya
wanachokisimamia’.
Zamani enzi zile Simba ikiwa na ‘ makomandoo’
mambo kama hayo yalikuwa yakifanyika, lakini
katika zama za sasa ambazo mchezaji
anasainiwa kwa mkataba, akilipwa mshahara,
atawezaje kuhujumu kazi yake ambayo
inamfanya mtu kama Kiemba mwenye mke na
watoto? . Hili haliwezi kuingia akili mwa mtu
mwenye ‘ fikra chanya’.
Huku ni kubomoa badala ya kujenga. Popote
pale duniani timu inapofanya vibaya, mtu
anayewajibika ni mwalimu na benchi lake la
ufundi na si mchezaji hata siku moja. Wachezaji
wangapi watafukuzwa kwa mtindo huo.
Chanongo anasimamishwa mara ya ngapi sasa?
Kwa nini inakuwa hivyo?. Mchezaji alicheza
vizuri ‘ inakuwa poa’, akishuka kidogo kiwango ‘
anahujumu’!!!
Post a Comment