Paka watatu wenye macho mekundu
walimshangaza Kamanda wa Polisi Kikosi cha
Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya
Tanzania, SACP Godfrey Nzowa pale
alipowakuta katika mlango wa ofisi yake na
kumng’ang’ania miguuni.
Sakata hilo lilitokea wiki iliyopita wakati
Kamanda Nzowa akitoka ofisini na mgeni wake
aliwakuta paka hao mlangoni.Kufuatia hali hiyo,
wageni na baadhi ya askari anaofanya nao kazi
walionekana kushangazwa na tukio hilo huku
wakijiuliza kwa nini paka hao wamzingire
kamanda huyo na kuwaacha watu wengine?
Hata hivyo, baadhi ya wageni waliokwepo
walihisi kuwa huenda paka hao walitumwa
kishirikina na watu anaopambana nao kwa
kuwakamata kutokana na kupatikana na
madawa ya kulevya kwani ameweza kwa kiasi
kikubwa kudhibiti biashara hiyo haramu hapa
nchini.
Akizungumza na Uwazi, askari mmoja alisema
Kamanda Nzowa amekuwa akipata vitisho na
majaribu ya kila aina ikiwemo rushwa lakini
kwa kuwa ni mcha Mungu mzuri anashinda.
Hadi wageni hao wanaondoka paka hao bado
walikuwa wamemng’ang’ania kamanda huyo.
Hata hivyo, kamanda huyo alirudi nyuma na
kufunga mlango na kuwaacha paka hao wakiwa
wamesimama nje ya mlango wa ofisi yake.
Mwandishi wetu alipomuuliza Nzowa kutokana
na hali hiyo alisema ni mambo ya kawaida
kwake na kinachomsaidia ni Mungu kwani kila
mara amekuwa akisali.
Chanzo: Uwazi
Post a Comment