Freemasons Walipasua kanisa la Anglikana

Sakata la baadhi ya waumini wa Kanisa Kuu la
Mtakatifu Nicholas Mwanza (DVN) kumkataa
Askofu Mkuu, Boniphace Kwangu wakimtuhumu
kuwa mwanachama wa imani ya Freemason
limechukua sura mpya baada ya baadhi ya
waumini juzi (Jumapili) kutotokea kanisani hapo
kwa madai kwamba mpaka hali ikae sawa.
Baadhi ya waumini hao ambao hawakutaka
majina yao yaandikwe, walisema wamepoa
majumbani mpaka uongozi utoe tamko
linalojulikana la sivyo watahamia makanisa
mengine kuliko kusali katika kanisa lenye
mgogoro wa kiimani.
Hivi karibuni, muumini mmoja wa kanisa hilo,
Msoma Lazaro alilazimisha kusoma tamko
madhabahuni kwa niaba ya kundi lake akisema
Askofu Kwangu haruhusiwi kuendesha ibada
kwenye kanisa hilo kuanzia siku hiyo.
Hata hivyo, wakati tamko hilo likisomwa na
Lazaro, kulizuka vurugu baina ya viongozi wa
kanisa hilo na msomaji wa tamko hilo wakizuia
lisisomwe kwa madai kuwa ni kuvuruga ibada
kwa sababu halikufuata utaratibu.
Akiwa katika harakati za kusoma tamko hilo,
baadhi ya viongozi walimzuia wakimtaka asubiri
kwanza, lakini kutokana na msimamo wake
alilisoma tamko hilo kabla ya kuondolewa kwa
nguvu na kuporwa karatasi ya tamko hilo
ambalo lilikuwa na baadhi ya picha za Askofu
Kwangu.
Uwazi lilifanikiwa kupata nakala ya tamko hilo
la kumkataa Askofu Kwangu likisema kuwa
ndiyo mwisho wake wa kutoa huduma zozote
za kiroho kanisani hapo na kwingineko
kutokana na mambo anayotaka kuyafanya
kanisani hapo yenye ishara za kishirikina
(Freemason).
Waumini waliompinga askofu huyo walisema
imethibitika kuwa ameonesha ukweli wa
kuondoa zuria (kapeti) ndani ya kanisa kwa
sababu za Freemason.
Alitaka kuchimbua vigae vya madhabahuni
akidai vimejengwa na kuwekwa hirizi na pia
ana mpango wa kufukua kaburi la askofu
hayati J. O. Rusbamayila aliyezikwa ndani ya
kanisa na kulipeleka nje ya kanisa.
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo walionekana
kumtetea Askofu Kwangu kwa kusema kuwa
wanaomwandamana ni mashetani wakubwa.
Mmoja wa waumini hao, mama Mataba alisema
picha zinazomwonesha askofu huyo akiwa na
mwanachama wa Freemason ni za kupandikiza
na za uongo, kwamba hawezi kujiunga na imani
hiyo hata siku moja.
“Picha ni za uongo.Tumekuja kusali na kuabudu
hatujaja kutoa tamko hilo hapa, hayo mambo
yanatoka wapi?” alihoji mama Mataba. Aidha,
mmoja wa waumini alisema pete inayovaliwa
na askofu huyo haina uhusiano wowote na
imani ya Freemason bali baadhi ya waumini
wanasema bila kujua pete ya Freemason ikoje.
Uwazi lilipozungumza na Askofu Kwangu kuhusu
tamko hilo lililosomwa kanisa hapo alisema
hajui chochote kwa sababu hakuhudhuria
ibada ya siku ya tukio kwa vile alikuwa kwenye
sherehe za kusimikwa kwa askofu wa Kanisa la
Africa Inland Church Tanzania ‘AICT’ ambaye
hakumtaja jina.
“Hili tamko limetolewa na nani, maana
sijahudhuria kanisani leo. Sisi tulikuwa kwenye
ibada ya usimikakwaji wa askofu mwenzetu.
Kama limepitia kwenye taratibu zetu
halijanifikia. Kama halikupitia katika njia hizo si
sawa, ni tamko la barabarani mtu kuota na
kutoa tamko,” alisema.
Akaongeza: “Naomba nisiwe na Comment katika
hilo na naomba usiniulize lolote, sielewi lolote
maana sikushirikishwa na sijasali hapo.”
Cedit: Uwazi/Gpl

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget