Kiongozi wa upinzani nchini Malaysia, Anwar
Ibrahim, amefika mahakamani kukata rufaa
dhidi ya hukumu inayomkabili kuwa alishiriki
ngono na mtu wa jinsia sawa.
Naibu waziri mkuu wa zamani aliyeshtakiwa kwa
kufanya mapenzi na mshirika wake mmoja wa
kisiasa alihukumiwa miaka mitano gerezani.
Bwana Anwar anadai kuwa mashtaka hayo
yalichochewa na maadui wake wa kisiasa.
Mamia ya wafuasi wake wamesongamana
mahakamani kuandamana dhidi ya hukumu
iliyotolewa dhidi yake.
Wafuasi wake wanaendelea kuuza tisheti
zilizoandikwa kuwa wanaitisha haki ya Bwana
Anwar.
Nje ya mahakama utadhani ni mkutano wa
hadhara wala sio kesi inayohusiana na uhalifu
wa mapenzi.
Ushoga ni haramu katika taifa hili lenye
Waislamu wengi lakini ni vigumu sana kupata
watu wameshtakiwa.
Mawakili wa Bwana Anwar wanatarajiwa
kuwasilisha mahakamani kuwa uchunguzi wa
DNA uliotumiwa ulivurugwa katika juhudi za
maadui wake wa kisiasa kumharibia sifa.
Maafisa wa Serikali wamekanusha kuhusika
katika kesi hiyo na wanasema kuwa kesi ya
Bwana Anwar imeshughulikiwa na Mahakama
huru.
Mwanasiasa huyo mkongwe ameshtakiwa kuwa
alifanya tendo la ngono na mshirika wake wa
kisiasa mwanamume.
Hili ni shtaka la pili la ushoga linalomkabili
Bwana Anwar tangu atimuliwe Serikalini mwaka
1998.
Post a Comment