Wakati nyota wa muziki wa Hip Hop, Rashid
Makwiro ‘Chid Benz’ akikamatwa Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa
na madawa ya kulevya akiwa njiani kuelekea
Mbeya, Rehema Chalamila ‘Ray C’ aliyekuwa
amemfungulia kesi ya kumpiga katika kituo cha
Polisi cha Oysterbay, amefuta shauri hilo na
kumsamehe.
Akiongea na Gpl, Ray C alisema ameamua
kumsamehe kwa sababu yeye ni mtu wa
Mungu na anaamini yanayomtokea ni ishara ya
kumtambulisha kuwa matumizi ya dawa za
kulevya hayafai.
“Mimi ni mtu wa Mungu, nimemsamehe na
wala sitaki kesi naye, lakini kumsamehe mimi
peke yangu hakusaidii, Watanzania wote kwa
pamoja tumuombee ili jambo hili limalizike na
likiisha, ninamuomba aje tushiriki pamoja katika
tiba ya Methadone,” alisema.
Ray C maarufu kama kiuno bila mfupa, alitoa
kauli hiyo muda mfupi baada ya kuandika
waraka katika akaunti yake kwenye mtandao
wa Instagram, akimsihi Chid Benz kuachana na
matumizi hayo ya madawa ya kulevya.
“Pole kaka yangu Chid Benz, naumia kuona
tatizo ulilokuwa nalo bado haujalitafutia jibu,
mimi ni dada yako na tumeshafanya kazi
pamoja. Tatizo ulilonalo na mimi nilishakuwa
nalo na niliweza kulitatua sababu nilijitambua
na kutafuta suluhu, nimejaribu kila njia
kukushauri badala yake ukaja na rungu la
kimasai na kunitandika nalo nyumbani
kwangu,” yalisomeka baadhi ya maandishi yake
mtandaoni.
Ray C aliendelea kuandika kuwa kitendo cha
kukamatwa kwake na madawa hayo kitakuwa ni
jibu zuri kwake kuwa anakoenda si salama na
kumtaka abadili njia na kuungana naye kwenye
tiba ya Methadone kwani ndiyo kiboko ya
madawa ya kulevya.
Chid Benz alikamatwa akiwa na kete 14 za
madawa ya kulevya pamoja na misokoto miwili
ya bangi
Post a Comment