Askari polisi wanne wamenusurika kulipuliwa
kwa bomu la kienyeji usiku wa kuamkia jana
lililotegwa eneo wanalokaa asakari hao.
Tukio hilo limetokea wakati wakikagua magari
jirani na transimita ya kituo cha TBC Songea
katika eneo la mshangano mkoani Ruvuma.
Hata hivyo polisi kwa kushirikiana jeshi la
wananchi wamefanikiwa kutegiua bomu hilo.
Kutokana na kishindo kikubwa wakati wa
kuliharibu bomu hilo mwanafunzi wa shule ya
jirani na lilikotegwa bomu hilo Malizia Konja
alizimia na anaendelea kupatiwa matibabu
katika Hospitali ya mkoa wa Ruvuma.
Tukio hilo linatokea zikiwa zimepita siku chache
baada ya askari polisi wawili kujeruhiwa vibaya
kwa bomu la kienyeji ambapo kamanda wa
polisi wa mkoa wa Ruvuma ACP Mihayo
msikhela anasema polisi kwa kushirikiana na
jeshi la wananchi wamefanikiwa kuliharibu
bomu hilo…
Muuguzi wa hospitali ya mkoa Agnes Charles
amethibitisha kumpokea mwanafunzi Malizia
Konja huku mwanafunzi huyo akieleza
ilivyokuwa baada ya kusikia kishindo cha bomu
hilo.
Post a Comment