Polisi nchini Africa Kusini wameonesha nyuso
zinazo dhaniwa kuwa ni wauaji wa golikipa na
kapteni wa timu ya taifa Africa Kusini Bafana
Bafana, Senzo Meyiwa.
Meyiwa alipigwa risasi na kufa siku ya jumapili
wakati alipokuwa akikabiliana na wavamizi
waloingia nyumbani kwa mpenzi wake Kelly
Khumalo ambaye ni mwanamuziki na pia ni
muigizaji,maziko ya Meyiwa yanatarajiwa
kufanyika mwishoni mwa wiki hii.
Kifo cha mwanasoka huyo kimeonesha picha
halisi ya kiwango cha uhalifu na matumizi
mabaya ya silaha nchini Africa Kusini.
Africa kusini inatajwa kuwa moja ya nchi zenye
matukio makubwa ya uhali,na kiwango cha
uhalifu kinazidi kuongezeka siku hadi siku.
Mwanzoni mwa mwezi huu mwanariadha Oscar
Pistorious alihukumiwa miaka mitano jela kwa
kosa la kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake.
Post a Comment