Rais Michael Sata wa Zambia aaga dunia

Familia ya Bwana Sata wameiambia BBC kuwa
Rais wa Zambia, Michael Sata, amefariki dunia
akiwa na umri wa miaka 77 katika hospitali ya
London alikokuwa akitibiwa ugonjwa ambao
haujatajwa.
Kifo chake kimetokea siku chache baada ya
Zambia kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa
nchi hiyo.
Mwanasiasa huyo mkongwe aliingia madarakani
mwezi Septemba 2011 baada ya kuongoza
chama chake cha Patriotic Front, na kumshinda
Rupiah Banda, ambaye alikuwa rais wakati huo
na chama chake cha Movement for Multi-Party
Democracy, kikiwa madarakani kwa miaka
ishirini.
Michael Chilufya Sata alizaliwa mwaka 1937
katika mji wa Mpika, eneo ambalo lilikuwa
wakati huo ni Northern Rhodesia. Muumini wa
dini ya Kikristo ya madhehebu ya Katoliki,
alifanya kazi kama afisa polisi, mfanyakazi wa
reli na mwanachama wa chama cha wafanyakazi
wakati wa utawala wa kikoloni. Baada ya
Zambia kupata uhuru wake, pia aliishi kipindi
fulani mjini London, akiwa mfanyakazi wa reli,
na kurejea Zambia, akiwa na kampuni ya teksi.
Akiwa mwenye sauti ya mkwaruzo yakiwa ni
matokeo ya kuvuta sigara kwa muda mrefu,
Bwana Sata aliibuka katika siasa na kupata
umaarufu katika miaka ya 1980.
Haraka akapata sifa ya kuwa gavana mwenye
kuchapa kazi kwa bidii, wakati akiongoza jimbo
la Lusaka na mtu wa utekelezaji kwa vitendo.
Lakini pia alijulikana kama mtu wa kutoa amri,
mtu asiyeendekeza urafiki na mkali- na
wapinzani wake walisema jina alilopewa la
bandia la "King Cobra" alikuwa anastahili kuitwa
hivyo.
Kwa mara ya kwanza alionekana kama mtu
ambaye angetekeleza ahadi za kupambana na
rushwa na kupata ufumbuzi wa tatizo la ajira na
kuleta ustawi wa jamii. Lakini kipindi chake
madarakani kiligubikwa na kuuzima upinzani wa
kisiasa na kudorora kwa uchumi.
Bwana Sata ni rais wa pili wa Zambia kufariki
dunia akiwa madarakani.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget