Kwa hali ya kushangaza, kituo cha television
cha matangazo cha tbc 1 kati ya vituo vinne
maarufu vya matangazo ya habari nchini
Tanzania kimeshika nafasi ya mwisho baada
ya kufanyiwa utafiti,
Kwa habari za uhakika ni kwamba kituo
kilichoongoza kuangaliwa na watazamaji
wengi ni ITV kikifuatiwa na Star TV, nafasi ya
tatu imeshikwa na Channel 10 na hatimaye
TBC1.
Kwa utafiti uliofanya na na TCRA imebainika
kuwa ni aibu kama kituo television ambacho
ni cha Taifa na ni UMMA kushika mkia nyuma
ya vituo binafsi jambo ambalo ni hatari.
Vyanzo vya kuaminika vinadai kuwa TBC1
imefikia hapi baada ya kugundulika inabagua
baadhi ya habari ya vyama vya siasa na
kutoa habari ya chama kimoja tuu jambo
ambalo siyo sahihi katika utashi wa
utangazaji na kutofuata uhuru wa
kiutangazaji ndani ya uongozi wa shirika la
habari la Tanzania,
Utafiti umeonyesha kuwa ili chombo cha
habri kiweze kuangaliwa na watu wote wa
vyama vyote ni lazima chombo cha habari
kitoe habari bila kubagua vyama vya siasa
maana watazamaji wana misimamo tofauti
na itikadi tofauti, na kama chombo cha
habari kikiamua kutoa habari kwa chama
kimoja cha siasa basi ujue hapo
watakaoangali hizo taarifa za habari ni hao
hao wa chama kimoja.
Watafiti pia walienda mbali zaidi na
kukinyoshea vidole kituo cha taifa cha
utangazaji kuwa ni chombo cha UMMA na
kisipende kubagua baadhi ya taarifa za
habari za vyama vya siasa kwa misingi ya
kuelekezwa na wanasiasa au viongozi wa
nchi maana madhara yake ni wananchi
kushindwa kuangalia hicho kituo.
Mwisho wake kitashindwa kufanya biashara
na hatimaye kutegemea tuu ruzuku serikalini
na hapo ndo nchi itazidi kupata hasara
badala ya kukiacha chombo kijiendeshe kwa
uhuru. Wametoa mfano kama shirika la
habari la Uingereza BBC lingefanya kama TBC
inavyofanya basi nayo ingeishia kutazamwa
tuu nchini uingereza na tena kwa watu
wachache tofauti na ilivyo sasa BBC
inatazamwa duniani kote.
Utafiti umeonyesha kuwa hivi vyombo vingine
vya habari ITV, Star TV na Channel 10
vimepata watazamaji wengi kwa kuwa
havibagui matangazo ya kada tofauti ya
vyama vya siasa na hapo ndoo inasababisha
waweze kupata watazamaji wa kutosha.
Post a Comment