Headlines
za dawa za kulevya ni miongoni mwa headlines ambazo zimekua zikitokea
kwenye vyombo vya habari Tanzania kila wakati na zimekua zikitaja au
kuhusisha baadhi ya watu maarufu, Wauzaji na hata watumiaji.
Headline nyingine ya leo Tanzania kuhusu dawa za kulevya imetokea
Bungeni Dodoma ambapo Waziri William Lukuvi aliwasha kipaza sauti baada
ya maswali ya mbunge Anne Kilango Malecela.
Alianza kwa kusema ‘Baada ya Wafanyabiashara wa dawa za kulevya
kukamatwa na dawa hizo ambapo uchunguzi ukishakamilika Watuhumiwa
hufikishwa kwenye vyombo vya sheria na kushitakiwa Mahakamani kwa mujibu
wa sheria, dawa za kulevya zilizokamatwa huifadhiwa na kutumika
Mahakamani kama vielelezo na baada ya kesi kukamilika dawa hizo
huaribiwa au kuteketezwa kwa amri ya Mahakama’
‘Uteketezaji wa dawa za kulevya umewahi kufanyika mwaka 2012 ambapo
kilo tisini na mbili (92) za Heroine ziliteketezwa katika kiwanda cha
Saruji Tanga ziliteketezwa kwa amri ya Mahakama na mwaka 2013 kilo mia
nne kumi na mbili za bangi na kumi na mbili za Heroine, kilo tano nukta
sita za Cocaine ziliteketezwa kwenye kiwanda cha Saruji Wazo Hill Dar es
salaam’
‘Zile
kesi ambazo zimechukua miaka mitatu au minne hazijaisha Mahakamani dawa
zao za kulevya tunazitunza na ndio maana mwaka huu kwenye bajeti
tumeomba MILIONI 300 kujenga jengo imara zaidi la kutunza dawa hizi na
mmeidhinisha, kwa hiyo dawa hizi nyingi bado tunazo kwa sababu tu kesi
zake hazijaisha, zinatakiwa zibaki mpaka amri ya Mahakama itakapotolewa’
Maelezo ya Waziri Lukuvi yanaendelea ambapo kwenye hii sentesi ya
tatu amesema ‘zoezi la kuteketeza dawa za kulevya ni shirikishi na
hufanyika chini ya usimamizi wa taasisi mbalimbali kama tume ya kuratibu
udhibiti wa dawa za kulevya, jeshi la Polisi, Mahakama, ofisi ya
Mwanasheria mkuu wa serikali, baraza la taifa la usimamizi wa mazingira,
Waandishi wa habari na taasisi nyingine husika’
‘Serikali imeshaandaa muswada wa sheria mpya kali zaidi itakayo ondoa
changamoto zilizokua zikijitokeza wakati wa matumizi ya sheria iliyokua
inatumika sasa, muswada wa sheria hii mpya utawasilishwa bungeni na
kusomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano huu unaoendelea’ – Lukuvi
Baada
ya haya maelezo ya Waziri Lukuvi, Anne Kilango alisimama na kuwasha
kipaza sauti kuuliza maswali mawili ya nyongeza…. akisema ‘Kwa nini
serikali inapokamata dawa za kulevya isichukue utaratibu wa kupeleka
zile kesi ndani ya siku kumi na nne na kutoa maamuzi kuliko sasa
zinavyochukua muda mrefu na kutoa mwanya wa hujuma ambazo Wananchi
wanahisi’
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu William Lukuvi akasimama na kuibu
kwa kusema ‘kwa niaba ya Mh. Waziri Mkuu, ni kweli sheria hii
inayotumika sasa ina upungufu mkubwa na kesi zinachukua muda mrefu sana
ikilinganishwa na nchi za wenzetu kama Bangladesh, sijakwenda lakini
nimesoma kwamba kwenye viwanja vyao vya ndege wameweka hata vituo na
hakimu wa zamu anakuwepo palepale Airport, akikamatwa mtu anaitwa hakimu
wa zamu anatoa hukumu kazi inaisha’
‘Kwa sheria yetu hii hata ukimuona mtu na dawa za kulevya haitoshi
mpaka ziende kwa Mkemia mkuu alafu upelelezi ufanyike, tunazo baadhi ya
hukumu mbalimbali zimetolewa vibaya pengine kutokana na sheria iliyopo,
matatizo tuliyonayo yote ni kwa sababu ya sheria hii’kwa hisani ya millardayo.com
Post a Comment