Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, virusi
vya ugonjwa hatari wa Ebola, vitadhibitiwa kikamilifu kufikia mwaka
ujao wa 2015. Umoja huo umesema, miezi michache ijayo kunaweza
kushuhudiwa kupungua maambukizi ya ugonjwa huo. Mratibu wa Umoja wa
Mataifa katika masuala ya Ebola, David Nabarro, amesema hayo na kuongeza
hata hivyo kuwa, bado hali ya mambo ni mbaya mno na kwamba jamii ya
kimataifa inatakiwa kujiandaa kukabiliana vikali na maradhi hayo kila
pale kutakaporipotiwa mwathirika wa Ebola. Ametaka kuongezwa juhudi
maradufu katika kupambana na ugonjwa huo hatari na kuonya kuwa, ikiwa
jamii ya kimataifa haitotoa ushirikiano wa maana katika suala hilo, basi
nchi zote za dunia zitalazimika kupambana na virusi vya Ebola kwa miaka
yote, suala ambalo litagharimu maisha ya watu wengi duniani. Kwa mujibu
wa Shirika la Afya Duniani (WHO), hadi sasa watu elfu 13 na 567
wamekwishaambukizwa virusi vya Ebola, huku watu wengine elfu tano wakiwa
tayari wamekwishapoteza maisha yao huko magharibi mwa Afrika.hisani ya radio teharan
Post a Comment