Kiongozi wa waasi afungwa jela nchini Kongo DRC
Mahakama ya kijeshi ya Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo imemuhukumu kifungo jela kiongozi mmoja wa waasi nchini humo.
Jenerali Jérôme Kakwavu ambaye ni mmoja wa viongozi wa zamani wa waasi
nchini humo, alihukumiwa jana na mahakama ya mji huo kifungo cha miaka
10 jela, kwa tuhuma ya kutenda jinai za kivita wakati akiwa kiongozi wa
waasi. Mahakama ya kijeshi ya mji huo imeeleza kuwa, Jenerali Jérôme
alishitakiwa kwa kufanya ukatili dhidi ya binaadamu, mauaji na mateso.
Habari zinasema kuwa, Jérôme alifanya jinai hizo mwaka 2003 na 2004
wakati alipokuwa kiongozi wa waasi katika mkoa wa Ituri, kaskazini
mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Katika upande mwengine
askari wa serikali ya Kongo kwa kushirikiana na wale wa kulinda amani wa
Umoja wa Mataifa MONUSCO, wameendelea na operesheni za kuwatia mbaroni
watuhumiwa wa mauaji ya hivi karibuni mashariki mwa nchi hiyo.teharan
Post a Comment