Bwana
Mujica ,aliyejulikana kama rais masikini duniani kutokana na maisha yake
,alisema kuwa ombi hilo lilitoka kwa kiongozi mmoja wa dini ya kiislamu
katika eneo la uarabuni.
Aliliambia gazeti la kila wiki la Busqueda kwamba iwapo atalikubali ombi hilo basi fedha hizo zitatumiwa kuwasaidia masikini.
Rais Mujika ambaye anajulikana kama Pepe anaishi katika shamba lake na hutoa pato lake kwa watu masikini.
Mnamo mwaka 2010 Mali yake ilikuwa inagharimu dola 1,800 ambayo ni bei ya gari lake la Volkswagen
Busqueda
liliripoti kwamba ombi la gari hilo lilifanywa katika mkutano wa
kimataifa mapema mwaka huu katika mji wa Santa Cruz Bolivia.
''Nilishangaa
mara ya kwanza ,a hivyobasi nikapuzilia mbali.lakini baadaye ombi
jengine lilikuja na hivyobasi nikaanza kulichukulia kuwa swala la
umuhimu'',. Alisema Mujika.BBC (V.S)
Post a Comment