Jumuiya ya Kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) imetaka kuchaguliwe
kiongozi wa kiraia wa serikali ya mpito nchini Burkina Faso ili
asimamie uchaguzi mwaka uajo, ikiwa ni baada ya rais wa muda mrefu wa
nchi hiyo Blaise Compaore kung'atuka madarakani wiki iliyopita.
Rais
John Dramani Mahama wa Ghana ambaye mwenyekiti wa sasa wa ECOWAS jana
aliongoza ujumbe wa jumuiya hiyo nchini Burkina Faso ili kusaidia mpango
wa kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia, baada ya jeshi kumteua
afisa wa ngazi za juu kuongoza nchi hiyo. Ujumbe huo uliojumuisha Rais
Goodluck Jonathan wa Nigeria na Macky Sall wa Senegal umefanya
mazungumzo na Luteni Kanali Isaac Zida, vyama vya upinzani, wafuasi wa
Compaore, viongozi wa kidini na makundi ya kiraia. Mahama amesema kwamba
makundi yote yametakiwa kuchagua wagombea watatu kwa ajili ya uteuzi wa
rais wa mpito na kwamba kipindi cha serikali ya mpito kitakuwa cha
mwaka mmoja.
Post a Comment