Awali dalili za homa hii zilionekana kama za ugonjwa wa ebola.kuvuja
damu, kutapika na joto kali la mwili.lakini kwa kuwa ebola ni ugonjwa
mpya, homa ya Lassa nayo bado ipo, ambayo inaelezwa kuwa kila mwaka watu
300,000 mpaka 500,000 huathiriwa na homa hii na watu mpaka 20,000
hupoteza maisha.
Kila nchi iliyoathiriwa na ebola pia ina ugonjwa
wa homa ya Lassa, ijumaa juma lililopita Dr.Geraldine O'Hara kutoka
Shirika la Madaktari wasio na mipaka MSF ameiambia BBC kuwa mmoja wa
wafanyakazi wenzake alipoteza maisha ingawa walifanya kila jitihada
kuokoa maisha yake.
Inaelezwa kuwa Nigeria huenda ikakumbwa na
mlipuko wa ugonjwa wa Lassa, wakati huu ikiwa ni majuma kadhaa baada ya
kufanikiwa kukabili ugonjwa wa ebola.
Kuna tofauti moja kubwa kati
ya ebola na homa ya Lassa.Lassa husababishwa na Panya ambao hubeba
vijidudu kwenye maeneo ya makazi ya watu na kwenye hifadhi za vyakula
hasa kipindi cha Kiangazi.
Profesa Robert Garry kutoka Chuo cha
Tulane amefanya utafiti kuhusu ugonjwa huu kwa amesema Kumekua na ripoti
kadhaa za watu kuugua homa ya Lassa nchini Sierra Leone.
Lassa huambukiza lakini si kila anayeambukizwa huwa katika hali mbaya, ugonjwa huu hausambai kwa kasi kama ebola.
Post a Comment